Vitu vikuu vitatu vinavyosababisha bawasiri

Vitu vinavyosababisha Bawasiri

Last Updated on 17/11/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Bawasiri ni nini?

Bawasiri au Kikundu au Puru ni hali ya kuvimba kwa mishipa ya damu katika njia ya haja kubwa. Kwa Kiingereza hujulikana kama Hemorrhoid au Piles.

Katika hatua yake ya kuonekana wazi ugonjwa hujitokeza kama uvimbe au vivimbe kadhaa kwenye maeneo ya tundu la haja kubwa.

Karibu katika kila watu wanne watu watatu kati yao wanasumbuliwa na ugonjwa huu. Ni ugonjwa wa pili kati ya magonjwa yanayosumbuwa watu wengi zaidi duniani baada ya U.T.I

Kutokana na sehemu au mahali hasa ugonjwa wenyewe unapojitokeza umepelekea watu wengi kuwa na aibu kujisema kwamba wanaumwa ugonjwa huu.

Tatizo la bawasiri linaonekana kuwawapata kirahisi zaidi wanawake kuliko wanaume.

Bawasiri husababishwa na nini?

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ugonjwa wa bawasiri husababishwa na nini.

Bawasiri ni ishara inayokuambia kwenye mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kuna kitu hakipo sawa.

Bawasiri ni tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Huu mfumo ukishakua mbovu unakupelekea kutokupata choo vizuri, unaanza kupata choo kigumu sana wakati mwingine unaweza kukaa siku kadhaa bila kupata choo kabisa.

Mfumo wako dhaifu wa mmeng’enyo wa chakula ndiyo sababu ya chakula kupita bila kumeng’enywa vizuri kwenye utumbo mdogo.

Hivyo chakula kinapitiliza kwenda moja kwa moja kama kilivyo kwenye utumbo mkubwa ambako maji maji ya kwenye chakula hufyonzwa na kuacha chakula kikiwa kikavu.

Utakapotaka kupata choo, choo hutokea kikiwa kikavu jambo linalokulazimu kutumia nguvu nyingi kukisukuma choo kitoke.

Nguvu hii unayoitumia wakati unapata choo ndiyo sababu ya kutanuka kwa misuli na kupelekea kukwanguliwa na choo kigumu na pole pole utaanza kuona kinyama kinajitengeneza, na kufuatiwa na maumivu na miwasho kwa ndani, na wakati mwingine unapata kilichoambatana na damu.

Unapoendelea kupata choo kigumu kwa kipindi kirefu misuli nayo huendelea kukwanguliwa na kinyama huongezeka mpaka kinatokea nje na kufanya bawasiri ya nje.

Ukiona unamaliza siku nzima hujapata choo au wakati mwingine inapita siku mbili au tatu au zaidi na hupati choo ni dalili mbaya sana kwa afya yako.

Vyovyote itakavyokuwa hakikisha kila siku unapata choo japo mara moja au mpaka mara tatu lakini isipite siku nzima hujapata choo.

Choo kiwe kilaini na usitumie nguvu nyingi ili kukipata na hata ikitokea choo kilaini sana tuseme unaharisha mara moja au mbili kwa wiki bado ni ishara una afya nzuri.

Choo unachopata kiwe ni kirefu ukubwa wa ndizi na kisiwe kinachokatikakatika kama kile cha mbuzi. 

Vitu vifuatavyo vinatajwa kama sababu zinazoweza kukusababishia ugonjwa huu.

Bawasiri kwa kawaida siyo kitu cha kutishia uhai wako lakini ni ugonjwa unaoweza kukufanya usijisikie vizuri karibu kila siku za kuishi kwako.

Ni ugonjwa wa kawaida na unawapata karibu nusu ya watu wote kabla hawajafikisha miaka 50.

Vitu vikuu vitatu vinavyosababisha bawasiri

1. Kukaa muda mrefu kwenye kiti

Kukaa muda mrefu kwenye kiti kama vile inavyowalazimu madereva wa magari ya masafa marefu au wale wanaofanya kazi za maofisini kila siku kunaweza kuwa ndiyo sababu ya kuvurugika kwa mmeng’enyo wa chakula.

Kujizuia kukaa muda mrefu chini au kwenye kiti kutakusaidia kupona bawasiri haraka kuliko kawaida.  

Ikiwa utaacha kukaa chini au kwenye kiti au ukapunguza pia kukaa chooni  muda mrefu, uwezekano wa kupata maumivu yatokanayo na bawasiri unapungua sana.  

Kukaa masaa matatu mfululizo unaangalia tu TV na umekaa chini, kwenye kiti au kwenye sofa ni jambo linaloweza kukusababishia bawasiri kirahisi sana.

Ni kwa sababu miili yetu haikuundwa kwa ajili ya kukaa. Unapokaa mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula hauwezi kufanya kazi zake vizuri na kwa kiwango cha juu kama inavyotakiwa na matokeo yake ndiyo bawasiri.

Kukaa muda mrefu kunaweza kuwa chanzo cha matatizo mengi ya kiafya ikiwemo uzito kupita kiasi, kitambi, kisukari, gesi kuzidi tumboni na kuathirika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Madhara ya kiafya yanayoletwa na kukaa muda mrefu kwenye kiti ambayo hupelekea kutokea kwa ugonjwa wa bawasiri ni pamoja na yafuatayo:

(a) Kupungua kwa mtiririko wa damu

Tunatambuwa kwamba mtiririko wa damu hupungua wakati tunapotumia muda mwingi katika siku tukiwa tumekaa tu iwe chini au kwenye kiti.

Na mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula ni kitu kimoja kati ya vingi vinavyoathirika na tabia hii.

Kwakuwa kitendo cha kukaa muda mrefu kinaziminya baadhi ya ogani na kupelekea mtiririko wa damu kupungua ni kawaida kwa mfumo wako wa utowaji taka mwili kuangamia.

Kukaa muda mrefu kwenye kiti ni moja ya sababu kuu ya mtu kupata tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana jambo ambalo ni chanzo cha matatizo mengi kiafya ikiwemo kukuletea ugonjwa wa bawasiri.

(b) Kuongezeka kwa shinikizo kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Jambo moja baya zaidi unafanya dhidi ya afya yako ni kukaa kwenye kiti baada ya kuwa umemaliza kula chakula.

Kukaa kwenye kiti baada ya kula kunapelekea chakula kumeng’enywa kwa pole pole sana tofauti na inavyotakiwa.

Wataalamu wengi wa afya wanahusisha kitendo cha kukaa muda mrefu kwenye kiti kinasababisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kupungua kasi yake na kukuletea matatizo zaidi ikiwemo gesi tumboni, kiungulia, mvurugiko wa tumbo na mwisho kabisa lazima upate bawasiri.

(c) Ugonjwa wa Moyo : Unapokuwa mtu wa kukaa tu damu inatiririka kidogo sana na mishipa inachoma mafuta kidogo kuliko inavyotakiwa kitu kinachosabbaisha asidi mafuta kujiunga kwenye mishipa ya moyo na kukupa wewe zawadi ya ugonjwa wa moyo.

(d) Ugonjwa wa Kisukari : Uwezo wa mwili wako kuitika kwa insulini unaathiriwa na kitendo chako cha siku moja tu ya kukaa masaa mengi kwenye kiti jambo linalopelekea kongosho lako kuzalisha insulini nyingi zaidi na mwisho wa hii ni wewe kupata ugonjwa kisukari.

(e) Saratani ya utumbo mpana (Colon Cancer): Kukaa muda mrefu kwenye kiti kunaweza kukupa uwezekano wa kupatwa na saratani ya utumbo mpana na saratani ya matiti.

Namna gani hasa yote haya yanakutokea haijulikani lakini inawezekana ni matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa insulin jambo linalohamasisha uongezekaji wa seli na ukweli kwamba kukaa tu kunaweza kukupunguzia uwezo wa mwili kutoa sumu na vijidudu nyemelezi vinavyoweza kukuletea saratani.

(f) Uzito kupita kiasi : Kukaa chini au kwenye kiti ndiyo sababu namba moja ya watu wengi kuongezeka uzito na unene kupita kiasi.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza mbona wanafanya mazoezi mbona wanafanya diet nab ado wanazidi kuwa na uzito mkubwa na hawapati majibu ya chanzo cha tatizo.

Ili mwili uchome mafuta lazima uwe umefunga kula au umefanya mazoezi ya viungo.

Kama hufungi kula na hufanyi mazoezi mwili hauchomi mafuta na badala yake mafuta yanazidi kurundikwa mwilini na kukuongezea wewe uzito na unene tatizo la kiafya ambalo linahusika moja kwa moja na kutokea kwa ugonjwa bawasiri.

Kukaa masaa mengi kwenye kiti ni aina mpya ya uvutaji wa sigara (sitting is a new smoking). Ukikaa chini au kwenye kiti masaa matatu mfululizo ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6.

Mambo Matano unayoweza kufanya ili kupunguza madhara ya kukaa muda mrefu kwenye kiti kuanzia leo

Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya kazi zitakulazimu ukae ndiyo ufanye kazi.

Kama wewe ni mmoja ya watu ambao kazi zako ni lazima zifanyike ukiwa umekaa masaa mengi kila siku unaweza kujaribu kupunguza madhara ya yatokanayo na kukaa muda mrefu kwa kufanya yafuatayo:

(a) Kama ni dereva

Kama ni dereva wa masafa marefu kwa mfano unaweza kuamua kupumzika kituo fulani kila baada ya masaa matatu na utumie kama nusu saa hivi ukiwa umesimama na ukitembea tembea kisha endelea na safari.

Siyo sahihi kiafya kwenda safari masaa mengi bila kusimama na kupumzika kidogo.

Vile vile jioni utakapopumzika tumia muda mwingi ukifanya mazoezi ya kutembea au kuchuchumaa na kusimama (squatting) ili kupunguza madhara ambayo yangeweza kukupata kama matokeo ya kukaa masaa mengi wakati wa kazi.

(b) Tumia vizuri muda wako wa mapumziko

Hata kama unafanya kazi ofisini bado kuna nyakati za mapumziko. Inawezekana ni muda wa kwenda kunywa chai (saa  nne asubuhi) na wakati wa chakula cha mchana (saa saba).  

Tumia muda huu kutembea tembea nje na ule chakula ukiwa umesimama.

Vile vile kama huwa unaletewa chakula mezani ofisini unaweza kubadili mfumo na ukawa unasimama mwenyewe kwenda mahali kinapopikwa ili upate nafasi ya kutembea na kusimama japo kwa nusu saa.

Kila unapopata nafasi ya kusimama na kutembea itumie vizuri nafasi hiyo hata kama ni kwenda chooni kupata haja ndogo.

(c) Weka alamu!

Kama unafanya kazi ofisini na unatingwa sana unaweza kuweka alamu katika simu au kwenye Kompyuta ili kwamba kila baada ya lisaa limoja au masaa mawili upate dakika kadhaa za kusimama kwa lazima bila kujali kuna nini unatakiwa kufanya.

(d) Fanya mazoezi

Kila asubuhi na jioni tumia dakika 30 mpaka 40 kila siku kufanya mazoezi ya kutembea, kukimbia au kuchuchumaa na kusimama (squatting).

(e) Staafu mapema

Fanya mpango wa kustaafu mapema kazi ya namna hii ili uwekeze kwenye afya yako mapema kabla mambo hayajawa magumu zaidi kiafya.

2. Ugali wa SEMBE

Sembe haifai kwa afya yako.

Ukoboaji wa mahindi kupitiliza unayafanya yapoteze nyuzinyuzi, madini na vitamini na wanga. Ambavyo ni vitu muhimu kwa kuutia mwili nguvu na afya.

Badala yake unga wa dona ndio unafaa kiafya na hasa kwako wewe unayeumwa bawasiri. Kwa sababu mahindi yanasagwa yakiwa na ganda lake. Pia kiini hakiondolewi ambacho ndio ‘target’ ya panya mharibifu.

Mchele mweupe pia haufai kiafya hasa kwa mtu mwenye bawasiri. Kwa sababu ukoboaji unafanya virutubishi kuondolewa.

Pia nyuzi nyuzi huondolewa.

Mchele huu mweupe unaweza kukufanya upate matatizo ya mmeng’enyo wa chakula tumboni.

Pia ulaji wa mchele huu haukupi lishe yeyote zaidi ya kujaza tumbo.

Badala yake unapaswa kula mchele wa kahawia.

Mchele huu una madini mengi na vitamini kwa ajili ya afya yako.

Bila kusahau ngano iliyokobolewa pia haifai.

Waweza kusema mbona unga huu unaongezewa vitamini na madini kiwandani? Chakula bora hakipatikani kiwandani. Wala hakihitaji kuongezewa virutubishi.

3. Kutokunywa maji ya kutosha kila siku

Maji ni uhai. Hili kila mtu analijuwa ila si watu watu wote wanafahamu umhimu wa maji mwilini. Kutokunywa maji mengi nay a kutosha kila siku ni sababu ya tatu katika sababu kuu zinazosabbaisha ugonjwa bawasiri kwa watanzania wengi.

Shida iliyopo ni kuwa kuna mtu hawezi kunywa maji mpaka asikie kiu. Kosa linaanzia hapa. Huhitaji kusikia kiu ndipo unywe maji. Kiu ni ishara iliyochelewa ya mwili kuhitaji maji.

Asilimia 75 ya mwili wako wote ni maji. Asilimia 85 ya ubongo wako ni maji.

Maji ndiyo kila kitu mwilini

Maji yanahusika moja kwa moja na mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula, kuzuia kufunga choo, uondowaji wa taka mwilini na kusafirisha viinilinishe toka sehemu moja ya mwili mpaka nyingine.

Kutokunywa maji mengi na ya kutosha kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni. Kumbuka nimesema maji ni uhai.

Haijalishi unaishi sehemu ya joto au sehemu ya baridi ni lazima unywe maji kila siku iendayo kwa Mungu kama unataka usipatwe na ugonjwa wa bawasiri.

Kila mtu ana kiasi chake cha maji anachohitaji kunywa kila siku kulingana na uzito wake. Tumia picha hii hapa chini kujuwa kiasi unachotakiwa kunywa kila siku kwa mjibu wa uzito wako.

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu bawasiri niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama unapenda kujifunza mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa bawasiri bonyeza HAPA.

SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Imesomwa na watu 976
Vitu vikuu vitatu vinavyosababisha bawasiri

3 thoughts on “Vitu vikuu vitatu vinavyosababisha bawasiri

  1. We are a group of volunteers and starting a new scheme
    in our community. Your web site offered us with
    valuable info to work on. You have done an impressive job and our entire community will be grateful to you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *