Vidonda vya tumbo na miguu kuwaka moto

Last Updated on 02/11/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

Vidonda vya tumbo na miguu kuwaka moto.

Kwenye makala hii naeleza kwa kirefu juu ya uhusiano uliopo kati ya vidonda vya tumbo na miguu kuwaka moto na miguu kuvimba.

Kuna baadhi ya wagonjwa wangu wa vidonda vya tumbo wamekuwa wakiniuliza iwapo vidonda vya tumbo ni moja ya sababu ya miguu yao kuwaka moto au hata kuvimba.

Napenda kukujulisha kuwa ni kweli Kabisa vidonda vya tumbo vinaweza kukuletea hali ya miguu kuvimba na kuwaka moto.

Labda unaweza kujiuliza uhusiano huo unakujaje kujaje hasa?

Vidonda vya tumbo na miguu kuwaka moto

Kwa sehemu kubwa vidonda vya tumbo vinaweza kuletwa mwilini kama matokeo ya asidi (tindikali) kuzidi mwilini.

Asilimia 80 mpaka 90 ya watu wanaougua vidonda vya tumbo ni matokeo ya asidi kuzidi katika miili yao, asilimia ndogo sana ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo vidonda vyao vimetokana na bakteria wa vidonda vya tumbo (H.pyrol).

Na hata kama vidonda vya tumbo kwa upande wako vimetokana na bakteria bado huyu bakteria naye ana kawaida ya kuleta hali ya uasidi mwilini.

Kwa hiyo kinacholeta miguu kuwaka moto ni hali ya asidi kuzidi mwilini kama matokeo ya vidonda vya tumbo.

Ishara za mwanzo kabisa za asidi kuunguzwa ndani katikati ya seli au kwa maneno mengine asidi kuzidi kwenye seli za mwili na madhara ya kijenetiki ambayo yanaweza kujionesha, ni maumivu mbalimbali yanayozidi kujitokeza katika mwili.

Kutegemea na kiasi cha asidi mwilini na namna na eneo lenyewe asidi ilipojijenga maumivu maalumu ya mwili hujitokeza.

Maumivu mengine yanayoweza kuletwa na vidonda vya tumbo ukiacha hayo ya miguu kuwaka moto ni pamoja na;

  • Kiungulia (heart burn)
  • Maumivu ya moyo (angina)
  • Maumivu sehemu ya chini ya mgongo (lower back pain)
  • Yabisi (rheumatoid)
  • Maumivu ya kichwa (migraine headaches)
  • Maumivu katika kiuno
  • Maumivu mbalimbali katika mishipa
  • Ganzi sehemu mbalimbali za mwili
  • Chembe ya moyo

Watu wengi siku hizi hawawezi kuishi wiki mbili au mwezi mmoja bila kumeza aina fulani ya dawa ya kupunguza maumivu.

Ni rahisi kuelewa namna gani maumivu ya miguu kuwaka moto yanavyoweza kujitokeza mwilini.

Ili kuuelewa mfumo wa utengenezwaji wa maumivu ya miguu kuwaka moto tunahitaji kwanza kujifunza namna usawa wa asidi na alkalini unavyofanya kazi katika mwili.

Vidonda vya tumbo na miguu kuwaka moto

Hali ya uasidi husababisha kuunguzwa kwa baadhi ya miishio ya neva mwilini.

Kunapotokea hayo, ubongo huonywa juu ya mabadiliko hayo ya kikemekali ya kimaeneo, ambayo sote hutafsiri kama MAUMIVU.

Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia miguu kuwaka moto.

Masaa 24 kwa siku seli zetu ndani ya mwili zinaunguza kaboni kama mafuta (cells burning carbon) ili kutuacha katika hali joto ya nyuzi joto 37.5.

Unapochoma kitu chochote, kinatoa nje taka moshi.

Taka zote hizo toka katika seli zote za mwili, lazima zirekebishwe muda wote wa masaa yote 24 kwa msaada wa matunda na mboga za majani.

Kwa afya bora kabisa, mwili unatakiwa kubaki katika hali ya 7.4 katika kipimo cha P.H (Potential Hydrogen).

Hali hii ya 7.4 PH huhamasisha afya kwa sababu ndiyo hali inayoviwezesha vimeng’enya vinavyofanya kazi ndani ya seli ambavyo hupata ufanisi mzuri katika P.H hii.

Ndani ya miili yetu, figo husafisha haidrojeni iliyozidi ambayo husababisha asidi toka katika damu na kuiweka katika mkojo.

Miguu kuwaka moto ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa kuwa alkalini.

Moja ya sababu kuu ya watu wenye vidonda vya tumbo kutakiwa kula matunda na mboga za majani kwa wingi ni kuwa vyakula hivi ni alkalini, wakati nyama, kuku, samaki, chipsi, ugali, tambi, wali, mkate, mayai, maandazi, chapati, soda na jusi zote za viwandani ni asidi.

Asilimia 80 ya mlo wa mtu kwa siku inapaswa kuwa ni mboga majani na matunda na asilimia 20 ndiyo iwe vyakula vingine.

Wengi wetu siku hizi tunakula vyakula ambavyo vimekwisha andaliwa tayari katika makopo au maboksi ai migahawa (fast food) na hatutumii vyakula vyenye alkalini ya kutosha.

Kumbuka kuwa kabonidayoksaidi ni asidi pia kama ilivyo kwa kahawa, chai ya rangi na pombe ambavyo huathiri PH ya damu na tishu.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na ukawa unajipima P.H ya mate na mkojo wako mara kwa mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye kuitunza 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Matokeo ya mwisho kabisa ya miguu kuendelea kuwaka moto kwa kipindi kirefu ni saratani ya miguu.

Kwa wewe unayesumbuliwa na maumivu ya miguu kuwaka moto na una vidonda vya tumbo unatakiwa ufanye kila uwezalo upone vidonda vya tumbo na hiyo hali ya miguu kuwaka moto itapotea yenyewe bila kupenda.

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu vidonda vya tumbo bonyeza hapa.

Imesomwa na watu 29
Vidonda vya tumbo na miguu kuwaka moto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *