Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri

Bawasiri husababishwa na nini

Last Updated on 17/11/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri

1. Kutokunywa maji ya kutosha kila siku

Tafiti zinasema kutokunywa maji ya kutosha kila siku kunaweza kukuletea ugonjwa wa bawasiri.

Kama haunywi maji mengi ya kutosha kila siku ni rahisi sana wewe kupatwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara na mwisho wake ni bawasiri.

Maji ni maji. Juisi, chai, soda au pombe haviwezi kuwa mbadala wa maji na tena vinywaji hivi vinaweza kukausha zaidi hata yale maji machache uliyonayo tayari mwilini.

Haijalishi uwe unaishi sehemu zenye joto au sehemu za baridi jizoeshe tabia ya kupenda kunywa maji mengi ya kutosha kila siku kwa mjibu wa uzito wako.

2. Kukaa tu chini au kwenye kiti masaa mengi

Kwenye dunia hii ya sasa ya kidigitali unaweza kupata vitu vingi ukiwa umekaa tu kwenye computer, simu au runinga (TV).

Wakati maisha yanaweza kuonekana rahisi kuishi kwa namna hii bado aina hii ya maisha inaweza kudhoofisha misuli ya mwili wako na kukuletea Zaidi bawasiri.

Unapokaa tu masaa mengi ni rahisi kuongezeka uzito na unene ni moja ya sababu kuu inayosababisha ugonjwa wa bawasiri.

Mazoezi ya viungo mara nyingi ni dawa ya uhakika kwa magonjwa mengi yatokanayo na tabia.

Kukaa mua mrefu kwenye kiti au chini kunavuruga na kuharibu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kukuletea magonjwa kama bawasiri, vidonda vya tumbo, gesi kujaa tumboni na mengine mengi yanayohusiana na tumbo.

Tazama TV kwa vipindi vile mhimu tu hasa taarifa ya habari, tofauti na hapo usitumie zaidi ya saa moja ukiwa umekaa tu ili kuepuka kuongeza zaidi tatizo la bawasiri.

3. Kula Zaidi vyakula feki

Kama unaishi mjini basi ni ukweli usiopingika kwamba unakula Zaidi vyakula feki (junk foods) na tena vingine vyenye kusisimua (spiced).

Vyakula hivi huongeza msukumo au presha sehemu ya eneo la misuli ya haja kubwa. Jambo hili linaweza kukuletea bawasiri au kuchelewesha uponyaji wa bawasiri uliyonayo tayari.

Vyakula feki ni vyakula vya madukani, vya kwenye makopo au vya kwenye migahawa (fast foods restaurants).

Pendelea kula vyakula vya asili zaidi na vinywaji vya asili zaidi kama unataka kupona haraka ugonjwa huu mbaya wa bawasiri.

4. Kushiriki tendo la ndoa kinyume na maumbile

Hii dunia sijuwi inaelekea wapi.

Kuna tabia mpya imeibuka kwenye kizazi cha sasa watu wanapenda kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile na wengine wanaimba mpaka nyimbo za muziki kabisa kujaribu kuhamasisha na kuwaonyesha wengine kwamba hilo ni jambo la kawaida.

Mapenzi kinyume na maumbile ni sababu nyingine inayokukwamisha usipone bawasiri yako kwa haraka na isijirudie tena.

Kwahiyo kama unataka kupona bawasiri amua kuachana na tabia hii mbaya haraka iwezekanavyo.

5. Kukaa muda mrefu chooni

Kama wewe ni mmoja wa wale ambao ukiwa chooni unaendelea kutumia simu na kuangalia picha facebook basi ujuwe unachelewesha uponyaji wa bawasiri yako bila kufahamu.

Kukaa muda mrefu chooni kunailazimisha damu kujaa na kusukumwa kwenye mishipa ya tundu la haja kubwa kitendo kinachoweza kuongeza uwezekano wa wewe kupatwa zaidi na bawasiri.

Ukienda chooni usiende na simu na usikae huko zaidi ya muda unaotakiwa kuwa huko na ukimaliza haja yako basi mara moja utoke.

6. Unapochelewa kwenda chooni

Kuna wakati inaweza kukutokea upo mbali kidogo na nyumbani na ukapatwa na hitaji la kutaka kupata choo lakini kwa sababu upo mbali na nyumbani unaweza kuamua kujizuia usiingie choo cha kulipia mpaka utakaporudi nyumbani.

Au wakati mwingine tu hata kama upo nyumbani unaweza kuwa upo bize na kazi au jambo fulani kiasi kwamba unapatwa na hitaji la kwenda chooni na bado hukimbii haraka kwenda chooni.

Kama utaendelea na tabia hii mbaya kwa kipindi kirefu inaweza kukuletea au kukuongezea zaidi uvimbe wa bawasiri na kama tabia hii haitadhibitiwa inaweza kukuletea dalili zenye maumivu za bawasiri.

7. Kutokula vyakula vya kutosha vyenye nyuzinyuzi kila siku

Vyakula vyenye nyuzi nyuzi ni mhimu na vya lazima hasa kwa mtu unayesumbuliwa na bawasiri.

Vyakula vyenye nyuzi nyuzi ni mhimu kwa ajili ya mwenendo wa kawaida wa tumbo.

Ukiona unapatwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara ni ishara hauli vyakula vyenye nyuz nyuzi vya kutosha kila siku.

Unapopata choo kigumu kinaweza kukuletea maumivu sehemu ya haja kubwa na kukuletea dalili za bawasiri.

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu bawasiri niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama unapenda kujifunza mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa bawasiri bonyeza HAPA.

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo:

Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri Share on X

SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Imesomwa na watu 1,065
Tabia 7 zinazokuchelewesha kupona bawasiri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *