Sababu kuu kwanini maziwa fresh ni hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Last Updated on 31/08/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Sababu kuu kwanini maziwa fresh ni hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Kunywa Maziwa fresh hakuwezi kukusaidia kupona vidonda vya tumbo.

Unaweza kupata nafuu kidogo baada ya kunywa maziwa lakini baadaye kidogo maziwa uliyokunywa yanakusababishia uundwaji zaidi wa asidi (tindikali) tumboni na kukuletea maumivu zaidi na ugonjwa kuongezeka.

Kwa miaka mingi wagonjwa wa vidonda vya tumbo walikuwa wakiambiwa wanywe maziwa fresh kwa madai kwamba ni dawa na ni kinywaji salama kwao.

Sayansi hubadilika kila mara.

Kile ulichojifunza na kuamini jana kinaweza kuja kuwa na ukweli tofauti kabisa kesho.

Kwa mfano mpaka karne ya 16 watu wote kote duniani waliamini kwamba jua linatembea na ndilo linaloizunguka dunia.

Baada ya tafiti kadhaa ndipo karne ya 16 mwanasayansi James Bradley mwaka 1725 akahitimisha na akaiambia dunia kwamba jua halitembei wala haliizunguki dunia, na kumbe kinachozunguka ni dunia na jua lipo limekaa sehemu moja.

Galilei Galileo ndiye aliyeanzisha ugunduzi huu mpya mwaka 1610.

Usiache kuendelea kujifunza kwani elimu ni bahari na haina mwisho.

Kwa hiyo tafiti za kisayansi za hivi karibuni zinasema maziwa fresh si salama kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Ukinywa maziwa fresh, maziwa huenda kutengeneza utando kwenye sehemu za tumbo zilizo dhuriwa na vidonda na hivyo kufanya maumivu haya ya tumbo kupungua kwa muda fulani, lakini maziwa hayo hayo huwa na tabia ya kusisimua uzalishwaji wa tindikali za tumboni (Hydrochloric acid) ambayo baada ya kuisha kwa utando uliotengenezwa na maziwa husababisha maumivu makali zaidi kwa mgonjwa.

Hii ndiyo sababu mgonjwa wa vidonda vya tumbo anapitia kipindi cha maumivu makali sana ya tumbo hasa saa chache baada ya kunywa maziwa fresh.

Hivyo, ukiwa na vidonda vya tumbo, usinywe maziwa fresh!

Kumbuka ni maziwa fresh ndiyo hutakiwi kunywa, kumbe mtindi unaotokana na maziwa ni salama kwako na unahimizwa kula mtindi mara nyingi kadri uwezavyo.

Mtindi una bakteria wazuri wanaohitajika tumboni kwako na husaidia kudhibiti bakteria wabaya wakiwemo wa vidonda vya tumbo

Mtindi pia huongeza sana kinga ya mwili

Kumbuka uwe ni mtindi ambao haujaongezwa vitu vingine ndani yake

Mtindi wa nyumbani au wa dukani yote ni sawa na unaruhusiwa kutumia kama unaumwa vidonda vya tumbo.

Pamoja na hayo yote ni mhimu kutambua kuwa hakuna aina fulani ya chakula inayoweza kukusaidia kuharakisha upone vidonda vya tumbo.

Kupona vidonda vya tumbo unahitaji dawa na uvumilivu kwani kwa vyovyote itavyokuwa bado haviwezi kupona haraka haraka kama baadhi ya watu wanavyotaka.

Ndiyo, kuna uwezekano baadhi ya vyakula vikawa vinaongeza zaidi tatizo au kuzuia uponyaji usifanyike kwa haraka

Inashauriwa pia mgonjwa wa vidonda vya tumbo asikae muda mrefu bila kula chakula na wakati huo huo asile milo mingi mara kwa mara ili kuzuia uzalishwaji wa tindikali kama matokeo ya mmeng’enyo wa chakula.

Kama umekuwa ukisumbuliwa na vidonda vya tumbo na umekuwa ukinywa maziwa fresh basi yaache na uniletee mrejesho hapa hali yako imeendeleaje baada ya miezi miwili ya bila kunywa maziwa.

Kumbuka pia lengo siyo kuishi na vidonda vya tumbo na wala lengo siyo ubaki mtumwa wa kuchagua ule nini na usile nini

Lengo ni ifike wakati huumwi tena, huishi tena na vidonda vya tumbo na huhitaji tena kuendelea kuwaza ule nini au usile nini.

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa vidonda vya tumbo niachie ujumbe WhatsApp +255714800175 au bonyeza HAPA.

Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine.

Ukipata muda soma pia na hii 👇

Vitu 6 nilivyojifunza kuhusu vidonda vya tumbo

Imesomwa na watu 3,148
Sababu kuu kwanini maziwa fresh ni hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *