Sababu kuu 2 kwanini huponi vidonda vya tumbo

Last Updated on 13/08/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Sababu kuu 2 kwanini huponi vidonda vya tumbo

Je vidonda vya tumbo vinatibika?

Vidonda vya tumbo vina dawa?

Vidonda vya tumbo vinapona?

Basi nimeshakutana na maswali ya namna hii kutoka kwa wasomaji wangu wengi kwa muda mrefu sana.

Hii inatuma picha kwamba kuna watu wengi tu hawafahamu au hawaamini kwamba vidonda vya tumbo vinapona au kutibika na kupotea na ikiwezekana visijirudie tena.

Mimi niliwahi kuugua vidonda vya tumbo mwaka 2013, hata hivyo kwa neema ya Mungu nilipona na sijaugua tena vidonda vya tumbo mpaka sasa.

Nayafahamu maumivu yake.

Tumbo linauma, linajaa gesi, unakosa usingizi, unapata choo kigumu cha mbuzi na wakati mwingine kimechanganyikana na damu.

Unaweza kutokewa na maumivu karibu kila sehemu ya mwili wakati wowote.

Mimi nilipona. Sijipi uhakika kuwa sitaugua tena lakini nilipona.

Wapo watu wanapona vidonda vya tumbo.

Wapo pia watu wengi sana ambao hawaponi vidonda vya tumbo.

Niseme tu ukweli watu wasiopona vidonda vya tumbo ni wengi.

Wengi wameamua kuufanya ugonjwa wa vidonda vya tumbo kuwa sehemu ya maisha yao.

Wamechagua kuishi na vidonda vya tumbo.

Wameshatumia dawa mbili, tatu hata tano tofauti na hawajapona.

Wamekata tamaa na matumaini.

Hawaamini kama kuna kupona vidonda vya tumbo.

Hizi hapa chini ni sababu kuu kwanini huponi vidonda vya tumbo

Soma pia makala hii

Dawa ya asili ya vidonda vya tumbo

Sababu kuu 2 kwanini huponi vidonda vya tumbo

1. Hujuwi vidonda vya tumbo vinatoka wapi

Huponi vidonda vya tumbo sababu hujuwi unavipata kutoka wapi.

Ukijua chanzo cha tatizo ni nusu ya kuwa umepata suluhisho la tatizo lako.

Vidonda vya tumbo unavipata kwa njia mbili.

A) Njia ya kwanza unapata vidonda vya tumbo ni kupitia kwa bakteria aitwaye H.Pyrol.

Bakteria huyu unaweza kumpata siku yoyote hata baada ya kuwa umepona vidonda vya tumbo.

Bakteria huyu unaweza kumpata na kukuingia tumboni kupitia chakula au vinywaji unavyokula na kunywa kila siku.

Kwahiyo, unaweza kuwa ulikunywa dawa ya vidonda vya tumbo na ukapona lakini baada ya muda kidogo au miezi kadhaa baadaye ukaugua tena.

Ukapona na ukaugua tena na tena na mzunguko huo ulipoendelea ukakata tamaa, ukafikia hitimisho kwamba vidonda vya tumbo haviponi na havina dawa.

Vidonda vya tumbo vinatibika, ila huyo bakteria bado yupo na anaweza kukuingia tena kupitia chakula au maji unayokunywa.

Na wewe ni lazima ule na unywe ndipo uishi.

Soma na hii pia

Uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo

B) Njia ya pili unavipata vidonda vya tumbo ni kupitia vyakula na vinywaji vyote unavyokula na kunywa kila siku.

Mara nyingi unapokula vyakula au kunywa vinywaji vyenye asidi (tindikali) nyingi vinaweza pia kukutoboa na kuleta vidonda kwenye kuta za tumbo lako.

Hii bdiyo sababu mgonjwa wa vidonda vya tumbo anahimizwa kupunguza ikiwezekana kutotumia kabisa vyakula au vinywaji vyenye asidi nyingi.

Hata vile vyakula visivyo na asidi nyingi ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo unahimizwa kula na kunywa navyo bado vinaweza kukuletea vidonda vya tumbo kutokana na hydrokloriki asidi inayotumika wakati wa mmeng’enyo wa chakula ambayo hutolewa kwa asili na mwili wenyewe dakika chache kabla hujaweka chakula mdomoni au ikiwa umepatwa na harufu ya chakula kizuri au umehisi njaa au umefikiri kutaka kula chakula fulani.

Kwa hiyo utagundua mpaka hapo kwamba karibu muda wote na siku zote mwili wako wenyewe unatengeneza vidonda vya tumbo au muda wowote unaweza kupata vidonda vya tumbo sababu ya bakteria kupitia chakula na vinywaji unavyotumia kila siku.

*Mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula karibu muda wote upo bize kukuletea vidonda vya tumbo.

*Kuna baadhi ya vyakula vinaleta vidonda vya tumbo kirahisi zaidi kuliko vyakula vingine.

*Hata vile vyakula visivyoleta vidonda vya tumbo bado navyo vinao uwezo wa kukuletea vidonda vya tumbo kupitia mchakato wa mmeng’enyo wa chakula kwa kuizarisha hydrokloriki asidi ili chakula unachokula kipate kumeng’enywa.

*Bado kuna bakteria anayeleta vidonda vya tumbo unaweza kumpata kupitia vyakula unavyokula kila siku.

Mpaka hapo unaweza kupata kufahamu kuwa wale waliokata tamaa kupona vidonda vya tumbo wapo sahihi na wala usiwabeze.

Soma na hii pia

Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula

2. Umeweka matumaini yako yote kwenye dawa na hela

Wapo baadhi ya watu matumaini yao yote kwenye kupona ugonjwa wowote wameyaweka kwenye hela wanayotoa wanaponunua dawa na dawa hiyo wanayopewa.

Kupona ingekuwa ni RAHISI hivyo matajiri wasingekuwa wanakufa.

Kuna juhudi nyingi nyuma ya pazia zinazofanyika zinazoonekana na zisizoonekana mpaka unapona ugonjwa fulani.

Kuna juhudi kadhaa lazima zije pamoja kwako ndipo utapona na siyo dawa au hela peke yake.

Ukitembelea hii blog yangu kurasa nyingi zaidi nimetumia muda mwingi zaidi kutoa dondoo, maelekezo, elimu, ufahamu mpya, msaada na kadharika.

Nina shuhuda za watu wengi ambao wamepona magonjwa mengi hata saratani kupitia maelezo yangu.

Kwahiyo kama wewe ukishatoa hela na ukapewa dawa ya vidonda vya tumbo unafikiri ndiyo umemaliza, nipo hapa kukuambia bado una safari ndefu kufikia uponyaji wako.

Hela haitibu mtu.

Hela ni kitu cha mhimu ili uonane na tabibu au upate dawa lakini kupona ni kitu kingine tena.

Wakati mwingine utakaponunua dawa ya vidonda vya tumbo muombe aliyekupa hiyo dawa akupe na maelezo mengine juu ya vitu vifuatavyo;

a) Vyakula na vinywaji ambavyo havina asidi nyingi mwilini

b) Vyakula na vinywaji vyenye asidi nyingi mwilini

c) Namna ya kuipunguza hydrokloriki asidi inayozarishwa tumboni wakati wa mmeng’enyo wa chakula isilete madhara ya kutoboa kuta za tumbo na kukuletea vidonda vya tumbo.

d) Mbinu nyingine nje ya vyakula na vinywaji za kupunguza asidi mwilini

e) Namna ya kumuua bakteria wa vidonda vya tumbo kwenye vyakula au vinywaji vya lazima unavyotumia kila siku.

f) Namna nzuri ya kudhibiti msongo wa mawazo (stress) kwenye maisha yako

Ikiwa unatafuta dawa nzuri ya uhakika ya asili inayotibu vidonda vya tumbo bonyeza HAPA.

SHARE POST HII NA WENGINE UWAPENDAO

Sababu kuu 2 kwanini huponi vidonda vya tumbo Share on X

Kabla hujaondoka soma hii pia

Vidonda vya tumbo husababisha upungufu wa nguvu za kiume

Imesomwa na watu 8,668
Sababu kuu 2 kwanini huponi vidonda vya tumbo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *