Madhara 9 ya vidonda vya tumbo mwilini

Madhara ya Vidonda vya tumbo mwilini

Last Updated on 12/06/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

Vidonda vya tumbo ni majeraha au vidonda ndani ya kuta za tumbo.

Majeraha au vidonda hivyo huleta maumivu yanayokera na hutokea mara nyingi tumboni na yanaweza kutibika lakini kama hutachukuwa hatua mapema za kutibu yanaweza kukuletea majanga mengine mengi kiafya.

Tumbo na utumbo mdogo vina kuta maalumu yenye ute ute wa ulinzi ambao hulilinda tumbo lako dhidi ya maadui wanaoleta shida tumboni mwako yaani bakteria wabaya, virusi na vijidudu nyemelezi vingine.

Wakati kuna vitu vingi vinavyoweza kukusababishia vidonda vya tumbo ikiwemo kutumia dawa za kupunguza maumivu kwa muda mrefu bila ushauri wa kitaalamu, kuvuta sana sigara au kunywa pombe kupita kiasi; kuna bakteria ambaye anaweza kulaumiwa kama mhusika mkuu wa vidonda vya tumbo.

Bakteria huyo anajulikana kama helicobacter pylori kwa kifupi H. pylori. Ni bakteria mwenye umbo la duara ambaye hushambulia ute ute wa ulinzi wa tumbo na sehemu ya juu ya utumbo mdogo.

Matokeo ya mashambulizi hayo ya huyu bakteria ni kutokea kwa vidonda kwenye kuta za tumbo na kuweka uwazi (vidonda) ambavyo hutumika kama njia ya kupitia bakteria wengine wabaya na kuongeza gesi tumboni.

Wakati hakuna uelewa wa moja kwa moja ni jinsi gani huyu bakteria anaingia tumboni, bado ni bakteria wa kawaida anayepatikana tumboni mwa watu wengi na anaweza kukuingia kupitia chakula na maji ya kunywa.

Tatizo la vidonda vya tumbo linalosababishwa na huyu bakteria ni kuwa anachelewa sana kukuonyesha dalili kwamba una vidonda vya tumbo.

Wakati unaweza kuishi na vidonda vya tumbo kwa muda fulani bila kukuletea shida kubwa, kuviacha kwa muda mrefu bila kupata matibabu kunaweza kukuletea madhara yafuatayo;

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

  1. Kuvuja damu ndani ya mwili (Internal bleeding and serious blood loss)
  2. Upungufu wa damu (Anemia)
  3. Kutapika damu
  4. Kupata kinyesi cheusi kama cha mbuzi
  5. Kuvurugika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (Obstructed digestion)
  6. Shida katika kupumua
  7. Saratani ya tumbo (Stomach cancer)
  8. Msongo wa mawazo (stress)
  9. Kupungua kwa nguvu za kiume

Ni mhimu kupata vipimo na uchunguzi zaidi wa daktari mapema tu unapohisi unaweza kuwa na vidonda vya tumbo ili kuzuia usipatwe na madhara haya yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo huwa ni rahisi kutibika unapowahi kuanza matibabu kuliko ukisubiri mpaka viwe sugu.

Soma hii pia > Uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini
Madhara ya vidonda vya tumbo

.

Vyakula hivi usile kama unaumwa vidonda vya tumbo

Kuna maelezo mengi juu ya vyakula kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Kuna wanaosema hiki hakifai wengine hiki kinafaa lakini kwa ujumla vyakula vifuatavyo vinakubalika na wengi kwamba havifai kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, navyo ni;

  • PiliPili Manga nyeusi na nyeupe
  • PiliPili kichaa
  • Vinywaji vyenye Kaffeine
  • Kahawa
  • Pombe
  • Chai ya rangi
  • Chokoleti na cocoa
  • Soda zote
  • Juisi zote za dukani
  • Sukari na viongeza utamu vingine vya kutengenezwa
  • Wali na ugali wa sembe
  • Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile maandazi nk (Fried foods)
  • Mnanaa (Peppermint)
  • Mbegu mbegu zenye Omega – 6
  • Maziwa fresh

Kuepuka vyakula hivi ni hatua moja kuelekea kwenye uponyaji wako hata hivyo unahitaji kubadili tabia zako zingine ikiwemo kuachana na msongo wa mawazo (stress) kwa gharama yoyote.

Iwe ni mtu ambaye una kawaida ya kuugua vidonda vya tumbo mara kwa mara au huumwi vidonda vya tumbo kwa sasa, kuviepuka vidonda hivi ni pamoja na kuhakikisha mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula unafanya kazi vizuri kwa kiwango chake cha juu kabisa.

Pia unaweza kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kwa kufanya yafuatayo:

  1. Kunywa maji glasi 2 (nusu lita) mara tu uamkapo kutoka kitandani kila siku. Kunywa tena kiasi hiki cha maji kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na cha jioni kila siku.
  2. Kula chakula kichache milo mingi. Kula hata mara 5 kwa siku lakini chakula kidogo kidogo siyo kingi kwa wakati mmoja.
  3. Kula pole pole ulapo chakula
  4. Hakikisha unapokula chakula huna mawazo mawazo (stress) yoyote.
  5. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzi nyuzi
  6. Kula vyakula vyenye bakteria wazuri (probiotics) kama vile mtindi na uji wa unga wa ndizi
  7. Punguza kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi

Hata kama utampata huyu bakteria (H. pylori) kama unao bakteria wengine wazuri tumboni ni rahisi kwako kumdhibiti huyu anayeleta vidonda vya tumbo.

Kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula ni jambo zuri kiafya siyo kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo tu bali kwa mtu yoyote asiyependa kuugua mara kwa mara kwani tumboni ndiko kuliko na injini ya mwili wote kwa ujumla.

H. pylori ni bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo kwa karibu ya zaidi ya nusu ya watu wote duniani hivyo uwezekano wa kumpata au kuugua ugonjwa huu ni mkubwa sana kwa mtu yoyote.

Kama unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa vidonda vya tumbo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Kama unapenda kujifunza mengi kuhusu vidonda vya tumbo bonyeza HAPA.

Ofisi yangu inaitwa *Tumaini Herbal Life* ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Madhara 9 ya vidonda vya tumbo mwilini Share on X

Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine

Imesomwa na watu 1,354
Madhara 9 ya vidonda vya tumbo mwilini

2 thoughts on “Madhara 9 ya vidonda vya tumbo mwilini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *