Dawa ya vidonda vya tumbo

Dawa za asili ya vidonda vya tumbo

Last Updated on 17/12/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Dawa ya vidonda vya tumbo.

Katika makala hii nitakueleza kiundani juu ya dawa ya vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo ni majeraha au vidonda ndani ya kuta za tumbo.

Vidonda vya tumbo husababishwa na nini?

Kwa kawaida vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria aitwaye Helicobacter pylori au kwa kifupi H. pylori.

Watu wawili katika kila watu watatu hapa duniani wana huyu bakteria tumboni mwao.

Na ingawa wengi wa watu hawa wenye huyu bakteria hawaonyeshi dalili yoyote ya kuumwa vidonda vya tumbo bado baadhi yao wanatokewa kuumwa.

Karibu asilimia 2 mpaka 20 ya watu wenye H. pylori wanaugua vidonda vya tumbo.

Wakati hakuna uelewa wa moja kwa moja ni jinsi gani huyu bakteria anaingia tumboni, bado ni bakteria wa kawaida anayepatikana tumboni mwa watu wengi na anaweza kukuingia kupitia chakula na maji ya kunywa.

Tatizo la vidonda vya tumbo linalosababishwa na huyu bakteria ni kuwa anachelewa sana kukuonyesha dalili kwamba una vidonda vya tumbo.

Wakati unaweza kuishi na vidonda vya tumbo kwa muda fulani bila kukuletea shida kubwa, kuviacha kwa muda mrefu bila kupata matibabu kunaweza kukuletea madhara makubwa kiafya.

Tunatambuwa pia asidi inahusika pia na kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Zaidi ya nusu ya watu wote wenye vidonda vya tumbo vidonda vyao ni matokeo ya asidi kuzidi mwilini na siyo H. pylori  bakteria moja kwa moja.

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH yaani potential hydrogen. Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Unaweza kukinunua kipimo cha PH na kupima Ph ya mate yako au ya mkojo wako kila mara ili kupata mwelekeo wa namna gani ufanye alkalini katika mwili wako ibaki kuwa ya 7.2 mpaka 7.4 kwenye seli ndani ya mwili wako.

Ikiwa mate yanasoma 6.0 au 6.5 ni kiashiria kuwa una asidi iliyozidi kwenye seli zako.

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Kadri unavyoendelea kuishi haidrokloriki ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.

Kila mtu anapaswa kula zaidi vyakula vyenye alkalini yaani matunda na mboga za majani na kunywa vinywaji vyenye asidi chache na ikibidi basi atumie vinywaji vyenye alkalini nyingi kama juisi ya limau, juisi ya chungwa, ya zabibu na maji halisi.

Hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo pia vinaweza kukutokea kama matokeo ya kutumia dawa za kupunguza maumivu kwa muda mrefu bila ushauri wa kitaalamu, kuvuta sana sigara au kunywa pombe kupita kiasi.

Jina langu naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili na ni Mtanzania.

Endelea kusoma ….

Dalili 17 za vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na

  1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
  2. Kuuma mgongo au kiuno
  3. Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
  4. Kizunguzungu
  5. Kukosa usingizi
  6. Usingizi wa mara kwa mara
  7. Maumivu makali sehemu ya mwili
  8. Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali
  9. Kichefuchefu
  10. Kiungulia
  11. Tumbo kujaa gesi
  12. Tumbo kuwaka moto
  13. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
  14. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
  15. Kukosa hamu ya kula
  16. Kula kupita kiasi
  17. Kusahahu sahau na hasira

Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali.

Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hufanyika hospitalini kwa kutumia mionzi au X-Ray kwa lugha ya kikoloni.

Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopi’ au ‘biopsi’, ambayo huyakinisha hali halisi.

Matibabu ya vidonda vya tumbo

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.

Soma hii pia > Vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kula

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

Vidonda vya tumbo ni majeraha au vidonda ndani ya kuta za tumbo.

Majeraha au vidonda hivyo huleta maumivu yanayokera na hutokea mara nyingi tumboni na yanaweza kutibika lakini kama hutachukuwa hatua mapema za kutibu yanaweza kukuletea majanga mengine mengi kiafya.

Tumbo na utumbo mdogo vina kuta maalumu yenye ute ute wa ulinzi ambao hulilinda tumbo lako dhidi ya maadui wanaoleta shida tumboni mwako yaani bakteria wabaya, virusi na vijidudu nyemelezi vingine.

Matokeo ya mashambulizi hayo ya huyu bakteria ni kutokea kwa vidonda kwenye kuta za tumbo na kuweka uwazi (vidonda) ambavyo hutumika kama njia ya kupitia bakteria wengine wabaya na kuongeza gesi tumboni.

Wakati unaweza kuishi na vidonda vya tumbo kwa muda fulani bila kukuletea shida kubwa, kuviacha kwa muda mrefu bila kupata matibabu kunaweza kukuletea madhara yafuatayo;

Madhara 9 ya Vidonda vya tumbo mwilini

  1. Kuvuja damu ndani ya mwili (Internal bleeding and serious blood loss)
  2. Upungufu wa damu (Anemia)
  3. Kutapika damu
  4. Kupata kinyesi cheusi kama cha mbuzi
  5. Kuvurugika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (Obstructed digestion)
  6. Shida katika kupumua
  7. Saratani ya tumbo (Stomach cancer)
  8. Msongo wa mawazo (stress)
  9. Kupungua kwa nguvu za kiume

Ni mhimu kupata vipimo na uchunguzi zaidi wa daktari mapema tu unapohisi unaweza kuwa na vidonda vya tumbo ili kuzuia usipatwe na madhara haya yatokanayo na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo huwa ni rahisi kutibika unapowahi kuanza matibabu kuliko ukisubiri mpaka viwe sugu

Soma hii pia > Uhusiano wa vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo

Jinsi ya kuimarisha mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula

Pia unaweza kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kwa kufanya yafuatayo

  1. Kunywa maji glasi 2 (nusu lita) mara tu uamkapo kutoka kitandani kila siku. Kunywa tena kiasi hiki cha maji kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na cha jioni kila siku.
  2. Kula chakula kichache milo mingi. Kula hata mara 5 kwa siku lakini chakula kidogo kidogo siyo kingi kwa wakati mmoja.
  3. Kula pole pole ulapo chakula
  4. Hakikisha unapokula chakula huna mawazo mawazo (stress) yoyote.
  5. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzi nyuzi
  6. Kula vyakula vyenye bakteria wazuri (probiotics) kama vile mtindi na uji wa unga wa ndizi
  7. Punguza kukaa chini au kwenye kiti masaa mengi

Hata kama utampata huyu bakteria (H. pylori) kama unao bakteria wengine wazuri tumboni ni rahisi kwako kumdhibiti huyu anayeleta vidonda vya tumbo.

Kuimarisha afya ya mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula ni jambo zuri kiafya siyo kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo tu bali kwa mtu yoyote asiyependa kuugua mara kwa mara kwani tumboni ndiko kuliko na injini ya mwili wote kwa ujumla.

H. pylori ni bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo kwa karibu ya zaidi ya nusu ya watu wote duniani hivyo uwezekano wa kumpata au kuugua ugonjwa huu ni mkubwa sana kwa mtu yoyote.

Dawa ya vidonda vya tumbo > Palimaua

Palimaua dawa ya asili ya vidonda vya tumbo na bawasiri

Unapotaka kutibu vidonda vya tumbo ni mhimu kutambua kwanza nini kinaweza kuwa ndiyo chanzo hasa cha tatizo kwa upande wako.

Watu wengi wanaugua vidonda vya tumbo kama matokeo ya kushuka kwa kinga zao za mwili jambo linalosababisha bakteria mbalimbali kushambulia na kutoboa tumbo.

Kadri hawa bakteria mbalimbali wanavyozidi kuongezeka tumboni wanaharibu mfumo wa kawaida wa uundwaji wa asidi mwilini na kupelekea asidi nyingi zaidi kuzalishwa zaidi ya inavyohitajika na mwili.

Asilimia 98 ya watu wengi wanaougua vidonda vya tumbo ni matokeo ya asidi nyingi kuzidi mwilini.

Palimaua ni dawa nzuri ya asili ambayo;

  • Inaongeza mara dufu kinga yako ya mwili
  • Inaua bakteria mbalimbali tumboni akiwemo bakteria wa vidonda vya tumbo H.Pyrol
  • Inaweka sawa usawa wa asidi na alkalini mwilini
  • Inarahisisha kutibu vidonda sehemu mbalimbali mwilini (ina vitamini C ya kutosha)
  • Inaondoa gesi tumboni
  • Inasafisha na kuondoa sumu mbalimbali mwilini
  • Inaondoa msongo wa mawazo (stress)
  • Inadhibiti virusi (anti-virus)
  • Inauongezea nguvu na ufanisi mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
  • Inaondoa uchovu sugu na kuongeza nguvu za mwili kwa ujumla
  • Inatibu maumivu na matatizo karibu yote ya tumbo ikiwemo bawasiri

Kama umeumwa vidonda vya tumbo kwa kipindi kirefu na umejaribu kila dawa bila mafanikio basi Palimaua ni suluhisho pekee la uhakika kwa tatizo lako.

Ni dawa ya uhakika kwa kutibu vidonda vya tumbo isiyo na madhara yoyote mabaya hapo baadaye.

Siyo vidonda vya tumbo tu utapona ukitumia dawa hii bali pia utaona afya yako ya mwili kwa ujumla imeimarika, utaona tu afya yako ni tofauti kabisa na ilivyokuwa hapo kabla hujaanza kutumia dawa hii.

Usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa Tabibu.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. 

Kama unahitaji Palimaua kwa ajili ya kutibu na kumaliza kabisa tatizo la vidonda vya tumbo kwenye maisha yako, niachie ujumbe WhatsApp +255714800175. 

Palimaua Inagharimu 55000 (elfu 55) ni ya kunywa kwa siku 30. 

Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni.

Kwa Dar Es Salaam tunaweza pia kukuletea mpaka ulipo kama utataka, hakuna gharama ya nauli (ni free delivery popote ndani ya Dar). 

Natuma pia popote ulipo nje ya Dar Es Salaam.  

Na ikiwa utanunua dawa ya asili kwa ajili ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo kutoka kwangu, nitakufundisha na vingine vifuatavyo BURE kabisa ;

1. Vyakula na vinywaji ambavyo mgonjwa anatakiwa kula kuanzia chakula cha asubuhi, cha mchana na cha jioni kwa siku 7 jtatu mpaka jpili.

2. Vyakula na vinywaji ambavyo havina asidi nyingi mwilini

3. Namna ya kuipunguza hydrokloriki asidi inayozarishwa tumboni wakati wa mmeng’enyo wa chakula isilete madhara ya kutoboa kuta za tumbo na kukuletea vidonda vya tumbo.

4. Mbinu nyingine nje ya vyakula na vinywaji za kupunguza asidi mwilini

5. Namna ya kumuua bakteria wa vidonda vya tumbo kwenye vyakula au vinywaji vya lazima unavyotumia kila siku.

6. Namna nzuri ya kudhibiti msongo wa mawazo (stress) kwenye maisha yako. Msongo wa mawazo ni moja ya sababu nyingine inayoongeza na kusababisha vidonda vya tumbo. 

SHARE POST HII NA WENGINE UWAPENDAO

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Dawa ya vidonda vya tumbo Share on X

Imesomwa na watu 17,600
Dawa ya vidonda vya tumbo

12 thoughts on “Dawa ya vidonda vya tumbo

    1. Hakuna bei ya jumla. inategemea tatizo lako lina muda gani na ni sugu kiasi gani. Tuwasiliane kwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *