Chakula cha mgonjwa mwenye vidonda vya tumbo

Last Updated on 10/11/2019 by Tabibu Fadhili Paulo

CHAKULA CHA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

Unachotakiwa ni kufanya utafiti au kujisomea mwenyewe sehemu mbalimbali aina ya vyakula na vinywaji vyenye alkalini nyingi, hivi ndiyo vyakula upendelee kula zaidi.

Wakati huo huo wewe mwenyewe binafsi jisomee huko na huko ni vyakula gani vina asidi nyingi na hivi ndivyo vyakula utakiwa uvikwepe kabisa au ule mara chache sana pengine mara moja tu kwa wiki.

Kwenye kila chakula chako cha kila siku visikosekane vitu 15 mpaka 20 kati ya vifuatavyo:

1. Kabeji
2. Asali
3. Ndizi
4. Nazi

5. Kitunguu swaumu > kinaua bakteria na virusi mbalimbali mwilini, kinaongeza kinga ya mwili, kinatibu majeraha, kinaondoa msongo wa mawazo (stress), kinatoa sumu mwilini.

6. Kitunguu maji
7. Mtindi
8. Njegere
9. Lozi
10. Brokoli
11. Karoti
12. Figili
13. Uyoga
14. Tango
15. Pilipili hoho nyekundu
16. Tufaa (apple)
17. Parachichi
18. Tende
19. Zabibu 
20. Embe 
21. Tikiti maji
22. Peazi
23. Chungwa
24. Mboga za majani karibu zote unaweza kula ila zisiive sana ukipika na ukiweza kupata unayoweza kula ikiwa haijapikwa ni vizuri zaidi.

25. Ndimu au limau. Ulifundishwa ndimu ni asidi? ndiyo mwalimu wako alikuwa sahihi ila aliiangalia ndimu ikiwa mkononi au kwenye chombo ila ndimu na hata limau ukinywa maji yake yanapofika tumboni hubadilika na kuwa alkalini tena alikalini nzuri inayohitajika na mwili kuliko hata ile ya kwenye mboga za majani.

Anza kidogo kidogo na uchanganye maji ya limau au ndimu na maji, maji ya limau kijiko kidogo kimoja cha cha chai changanya na vijiko vikubwa vitano vya maji na unywe kutwa mara 2 kila baada ya chakula. Ndimu au limau au machungwa ni matunda yenye vitamini C. Vitamini C ni mhimu ili kuongeza kinga yako ya mwili, kuondoa sumu mwilini, kutibu majeraha na vidonda.

Ndiyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaruhusiwa kutumia ndimu au limau.

26. Tangawizi > Inaua bakteria, kinatibu majeraha na vidonda, inaondoa sumu mwilini, dawa kwa zaidi ya magonjwa mengine 48 mwilini. Anza kidogo kidogo usiweke kiasi kingi na unaongeza kuchanganya na juisi zingine za matunda au supu za mboga mboga ili kupunguza ukali wake. Ndiyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaruhusiwa kutumia tangawizi.

27. Maji ya kunywa

28. Ufuta
29. Mayai > ya kienyeji

VYAKULA HIVI KULA MARA CHACHE SANA

30. Unga wa ulezi 
31. Ugali wa dona
32. Mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread)
33. Binzari/manjano
34. Viazi vitamu > vya kuchemsha vizuri zaidi
35. Nyanya
36. Wali > uwe wali wa nazi mara 2 au 3 tu kwa wiki.
37. Samaki
38. Kuku > wa kienyeji 
39. Nyama

Kama unaweza kuandaa mlo (recipe) kupitia majina ya vyakula (ingredients) nilivyoandika hapo juu hasa mpaka vyakula namba 29 kielezee hicho chakula hapo chini kwenye comment mahitaji na namna kinavyoandaliwa na utuambie pia kinaliwa muda gani hasa kama ni cha asubuhi, mchana au jioni au wakati wowote.

Nitavieleza hivyo vyakula kimoja baada ya kingine hapa chini;

MAJI YA KUNYWA NI MHIMU SANA KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

Kuna maajabu zaidi ya milioni moja kwenye glasi moja ya maji ya kunywa. Maji ndiyo dawa ya kwanza ya mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Ikiwa unaumwa vidonda vya tumbo na hufanyi bidii kunywa maji ya kutosha kila siku itakuwa ni vigumu kwako kupona vidonda vya tumbo hata ukipewa dawa kutoka wapi.

Ingawa wengi tunatambua vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria, lakini tafiti zinasema zaidi ya asilimia 80 ya watu wanaougua vidonda vya tumbo chanzo cha ugonjwa huu kwao siyo bakteria bali ni matokeo ya asidi kuzidi mwilini ndiyo maana hata tunapozungumzia vyakula vya mgonjwa wa vidonda vya tumbo akili yetu yote tunaiweka zaidi kwenye kukwepa vyakula au vinywaji vyenye asidi sana.

Maji ni uhai.

Bila kunywa maji ya kutosha kila siku ni sawa na mtu aliyeenda kupata mahitaji dukani lakini hana hela mkononi. Mwili hauna sehemu ya kuyahifadhi maji kwa matumizi ya kesho hivyo tunapaswa kunywa maji kila siku.

Tunapaswa kunywa maji bila kusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwisho kabisa ya mwili kuhitaji maji.

Haijalishi unaishi mazingira ya baridi au ya joto kama mgonjwa wa vidonda vya tumbo lazima unywe maji mengi kila siku kuanzia lita 2 mpaka 3 kidogo kidogo kutwa nzima.

Wakati wa lazima kabisa kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo kunywa maji ni nusu saa au robo saa kabla ya chakula.

Mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni marufuku kula chakula kabla hujanywa maji nusu saa au robo saa kabla.

Kwanini mgonjwa wa vidonda vya tumbo anywe maji kabla ya chakula? Nimesema asidi ndiyo inahusika na kuleta vidonda vya tumbo kwa watu kwa zaidi ya asilimia 80.

Unapotaka kula chakula au macho yako yakikiona chakula au pua yako ikisikia harufu ya chakula au kichwani kwako ukiwaza mambo ya chakula au kula chakula fulani, tumboni kwako huwa kunazalishwa maji maji ya asidi yajulikanayo kama haidrokloriki asidi.

Hii haidrokloriki asidi lazima izalishwe tumboni ili kuaanda mazingira ya chakula unachowaza au kutaka kula kiweze kumeng’enywa vizuri na tumbo.

Hii asidi ni kali na inatakiwa ipunguzwe makali kabla hujaanza kula chakula. Na inapunguzwa makali kwa wewe kunywa maji robo lita robo saa au nusu lita nusu saa kabla ya chakula.

Ikiwa hii asidi haitapunguzwa makali basi pole pole kadri miaka inavyosogea unapoendelea kula chakula bila kunywa maji kwanza inatoboa kuta za tumbo kidogo kidogo na hivyo kusababisha majeraha na vidonda vya tumbo tumboni.

Shida ilianzia pale ulipoambiwa na kukaririshwa kwamba ukisikia kiu ndiyo unywe maji. Kumbe huhitaji kusubiri au kusikia kiu ndipo unywe maji.

Unapaswa popote ulipo iwe kazini, shambani, nyumbani, popote ulipo uwe na chupa yako ya maji pembeni kwamba wakati wowote unaweza kunywa maji kidogo na siyo mpaka utakaposikia kiu ndipo ukayatafute maji.

Inasisitizwa pia maji ya kunywa yawe katika joto la kawaida (room temperature) yasiwe maji ya baridi ya kwenye friji.

Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji. Maji ni uhai, hakuna maji hakuna maisha chini ya jua.

Maji ni mhimu zaidi kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo mara 10000 zaidi kuliko dawa ya aina yoyote ya vidonda vya tumbo utakayoandikiwa au kupewa na daktari yoyote kutoka popote duniani.

Kwa ufupi maji ni mhimu sana ili kupunguza, kuzuia na kuondoa asidi mwilini. Maji ni mhimu ili kuwa na mmeng’enyo wa chakula unaofanya kazi kwa ufanisi mzuri zaidi. Maji ni mhimu ili kulinda na kuimarisha kinga ya mwili, maji yanaondoa sumu mwilini kirahisi zaidi kuliko dawa nyingine yoyote ya kuondoa sumu mwilini uliyowahi kuisikia.

Haijalishi upo Arusha, upo Mbeya au upo Njombe au upo Dar Es Salaam jiwekee utaratibu wa kunywa maji kila siku lita 2 kwa mtu mwenye uzito mpaka kg 70 na lita 3 kwa mtu mwenye uzito kuanzia kg 80 kwenda juu. Usizidishe kunywa maji zaidi ya lita 3 kwa siku bila muongozo au ruhusa ya daktari wako wa karibu.

Usinywe maji mengi kwa pamoja zaidi ya nusu lita. Kunywa maji mengi kwa wakati mmoja ni hatari kwa afya yako. Kunaweza kusababisha madini na vitamini nyingi mhimu kupotea kirahisi mwilini kwa njia ya mkojo na kukuletea madhara zaidi kuliko faida.

Kila baada ya masaa mawili mtu anaweza kunywa maji glasi moja na asipatwe na madhara yoyote.

Kama utahitaji maelezo zaidi juu ya uzito wako na kiasi cha maji unachotakiwa kunywa na kwa wakati gani na gani hasa unaweza kunitafuta binafsi (private) kwenye WhatsApp +255714800175

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI

Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyue wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Mwisho jipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.

Makala hii inaendelea kuboreshwa, endelea kuja

SHARE NA WENGINE UWAPENDAO

Imesomwa na watu 15,960
Chakula cha mgonjwa mwenye vidonda vya tumbo

8 thoughts on “Chakula cha mgonjwa mwenye vidonda vya tumbo

    1. Kanuni ya jumla ni asilimia 80 ya chakula chako kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. wewe utapanga kuona asubuhi ule matunda au jioni ule matunda. Asilimia 20 vyakula vingine vya kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *