Last Updated on 10/02/2024 by Tabibu Fadhili Paulo
Jinsi ya kupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo
Kwenye makala hii naeleza kwa kirefu juu ya nini na nini hasa unaweza kufanya ili kupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo pale yanapokutokea.
Aidha niseme mapema kwamba lengo lako kuu lisiwe kwenye kupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo tu bali kuvitibu na kuondokana navyo kabisa vikae mbali na maisha yako.
Hakuna sababu yoyote ya kuendelea kuishi na kubembelezana na vidonda vya tumbo mwaka hadi mwaka wakati dawa za asili za kumaliza tatizo hilo zipo.
1. Kunywa mtindi
Mtindi unao bakteria wazuri ambao wanaweza kusaidia kurejesha usawa tumboni na kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Kuna bakteria wa aina mbili mwilini ; bakteria wazuri na bakteria wabaya.
Kwa kawaida mara nyingi sababu ya mitindo ya vyakula na vinywaji tunavyotumia kila siku tunajikuta idadi ya bakteria wabaya inakuwa kubwa kuliko ile ya bakteria wazuri.
Unapotokewa na maumivu tumboni sababu ya vidonda vya tumbo ni dalili mojawapo kwamba bakteria wabaya wamezidi.
Mtindi hauna uwezo wa kumuua bakteria anayeleta vidonda vya tumbo (H. Pylori) lakini utakusaidia kukuongezea idadi ya bakteria wazuri na hivyo kuongeza kasi ya kupona na kutuliza maumivu ya vidonda vya tumbo.
Ikumbukwe hapa nazungumzia mtindi na ndiyo ninaosisitiza kwamba mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia kupunguza maumivu lakini wakati huo huo nakukataza kwamba usinywe wala usitumie maziwa fresh kama wewe ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Kama unaweza kuandaa mtindi nyumbani wewe mwenyewe ni vizuri zaidi lakini hata ule wa dukani nakuruhusu unaweza kutumia.
Ukisikia maumivu ya vidonda vya tumbo yanakujia unaweza kunywa kikombe kidogo kimoja cha mtindi (robo lita) na maumivu hayo yatakuacha.
2. Kula kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu ni kiungo maarufu sana kwa vyakula popote duniani.
Kila chakula kinachopikwa sambamba na kitunguu swaumu lazima kiwe kitamu ingawa bado kuna wapishi wazembe wasiojua umhimu wake.
Kitunguu swaumu kinazo nguvu dhidi ya bakteria na virusi, hii ni sifa ambayo inakipa uwezo wa kupambana na maambukizi mbalimbali mwilini.
Baadhi ya tafiti zinakubali kwamba kitunguu swaumu kinao uwezo wa kumuua bakteria wa vidonda vya tumbo na baadhi ya tafiti zinakataa.
Hata hivyo kitunguu swaumu kinao uwezo wa kuzuia kuongezeka zaidi kwa vidonda vya tumbo na kusaidia mlolongo wa uponyaji.
Utafiti mmoja wa mwaka 2015 ulihitimisha kuwa kitunguu swaumu kinao pia uwezo wa kuzuia kuendelea kuongezeka kwa bakteria wa vidonda vya tumbo (H. Pylori).
Kingine kinachosababisha kitunguu swaumu kiwe kizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni ule uwezo wake wa kuongeza sana kinga ya mwili.
Mara nyingi kinga yako ya mwili inapokuwa vizuri husumbuliwi na magonjwa mengine kirahisi rahisi ikiwemo vidonda vya tumbo.
Kitunguu swaumu pia husaidia kupunguza gesi tumboni kirahisi zaidi jambo ambalo ni mhimu sana kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Sasa, ingawa ni vizuri sana kuwa na tabia ya kupenda kupika vyakula vyako huku ukiongeza na kitunguu swaumu, bado utapata matokeo mazuri zaidi iwapo utakitumia kikiwa kibichi yaani bila kukipika kwenye moto.
Ukitokewa na maumivu ya vidonda vya tumbo kula punje 2 za kitunguu swaumu wakati unakula chakula cha mchana na cha usiku.
Kwa vile wewe ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo nakushauri utumie kitunguu swaumu wakati tu unapokula chakula na siyo kitunguu swaumu peke yake.
Hivyo iwe unakula ugali wako na mboga za majani basi katikati wakati unaendelea kula chakula chukua punje 2 menya, tafuna kisha kula chakula chako.
Usitumie kitunguu swaumu tofauti na maelezo haya hasa kama wewe ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
3. Lamba asali
Asali ni kiongeza utamu cha asili kisicho na madhara na kinachotumika na kuheshimiwa kote duniani.
Asali huwa haiozi wala kuharibika.
Mara nyingi sana nimeandika kwamba ni mhimu sana kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo kupenda kutumia asali kwenye vyakula na vinywaji vyake kama mbadala wa sukari.
Watu wanaopenda kutumia asali wanaweza kufaidika na faida zake nyingi kiafya ikiwemo hili la kupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo.
Asali nzuri, Safi na mbichi inao uwezo dhidi ya bakteria wa vidonda vya tumbo (H. Pylori).
Wataalamu wengi wanasema asali inaweza kuwa msaada mkubwa sana kwenye kuzuia, kutibu na kupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo.
Asali inaweza pia kutumika kurahisisha uponyaji wa majeraha na vidonda hata juu ya ngozi ya binadamu sababu hufukuza mbali bakteria wowote wabaya.
Inaongeza kinga ya mwili, inaongeza nguvu ya mwili.
Ukisikia maumivu ya vidonda vya tumbo lamba asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula kila baada ya masaa manne mpaka urudi kawaida.
Ingawa asali ni tamu na ni nzuri kwa afya, bado hutakiwi kuitumia kwa fujo au kwa wingi kwa wakati mmoja kwani ina madhara yake ikizidi.
4. Kunywa maji
Namna nyingine rahisi sana na isiyo na gharama yoyote ya kupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo ni kunywa maji.
Hii ni dawa ya bure ya kupunguza maumivu ambayo wengi hawaifahamu ingawa wanayo mikononi mwao muda wote!
Hata hivyo usijali sana kwakuwa hatimaye leo utapata maelezo yake hapa kwangu bure.
Bila shaka umeshasikia mara nyingi watu wakisema kuwa maji ni uhai ila tu huwa unadhani wanaposema hivyo wanamaanisha ni ule uwezo wa maji kukuondolea kiu unapokuwa umebanwa nayo!
Ni kweli maji ni uhai na hakuna maisha popote bila maji.
Asilimia 75 ya mwili wako wote ni maji, asilimia 85 ya ubongo wako ni maji, asilimia 27 ya mifupa yako ni maji na asilimia zaidi ya 90 ya mtoto anayezaliwa ni maji
Siwezi kuandika kwa maneno ya kawaida ukaelewa ni jinsi gani maji ni mhimu sana kwa afya yako
Maji yanayo uwezo wa kuweka Sawa usawa wa tindikali (asidi) na alkalini mwilini, hali ambayo ni mhimu sana kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Tunatambua kwamba karibu asilimia 80 ya watu wanaoumwa vidonda vya tumbo vidonda vyao ni matokeo ya asidi kuzidi tumboni na siyo matokeo ya bakteria wa vidonda vya tumbo (H. Pylori).
Ukiacha maji ya kunywa na mboga za majani ambavyo ni alkalini, karibu vyakula na vinywaji vingine vyote vilivyobaki ni asidi (tindikali inayotoboa kuta za tumbo na kuleta vidonda).
Kwahiyo maji ya kunywa ni msaada mkubwa sana katika kutuliza maumivu ya vidonda vya tumbo.
Unachotakiwa kufanya ukisikia maumivu ya vidonda vya tumbo ni kunywa maji kikombe kimoja (robo lita) kila baada ya masaa matatu mpaka maumivu yatakapokuacha.
Vile vile jijengee utaratibu wa kunywa maji kikombe kimoja kila robo saa kabla ya kula chakula au maji vikombe viwili kila nusu saa kabla ya chakula, hii itakusaidia kudhibiti asidi inayotengenezwa muda mchache tumboni mwako kabla ya kula ili kuusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kumeng’enya chakula unachotaka kula.
Asidi hiyo huzalishwa pia kila ukisikia harufu ya chakula, ukiona chakula au ukihisi kutaka kula chakula.
Ni mhimu maji yasiwe ni maji ya kwenye friji, bali maji yenye joto la kawaida (room temperature).
5. Dhibiti msongo wa mawazo
Moja ya vitu vinavyoweza kuamsha maumivu ya vidonda vya tumbo ni kuongezeka kwa msongo wa mawazo maarufu kama ‘stress’.
Msongo wa mawazo unaweza kuzidisha zaidi maumivu na vidonda vya tumbo mwilini mwako.
Jaribu kuangalia ni nini hasa ndiyo chanzo cha stress kwenye maisha yako na fanya kila uliwezalo kukiondoa.
Baadhi ya misongo ya mawazo inaepukika na baadhi inakuwa ngumu kuepukika sababu ya imani na ulivyoaminishwa na watu wengine kwamba maisha lazima yawe hivi kumbe hakuna ulazima wowote wa kuishi kwa misingi hiyo.
Linapokuja suala la kulinda afya yako hasa afya ya akili haijalishi nani anasema au kuwaza nini juu yako, bali uwe tayari kwa lolote mhimu mwisho wa siku ubaki salama.
Wewe mwenyewe ndiyo mtu wa kwanza na wa mhimu zaidi kuliko mwingine yoyote kwenye maisha yako
Sisemi usiwajali wengine, ninachosema usiwe tayari kuhatarisha maisha yako na afya yako kwa ajili ya wengine ambao hawaonyeshi dalili yoyote kukujali wewe.
Wakati huo huo unaweza kudhibiti baadhi ya misongo ya mawazo kwa kupenda kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara, kuhudhuria kanisani au msikitini mara nyingi, kujichanganya na marafiki, kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara nk
Haijalishi ni nini ndiyo chanzo hasa cha msongo wako wa mawazo, tambua unao uwezo wa kufanya kitu fulani ili kubadili hali yako.
Ikiwa umekuwa ukikabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo (stress) kwa muda mrefu na huoni kabisa suluhisho la tatizo lako unaweza kuonana na mimi kwa msaada zaidi, nitafute kwenye WhatsApp +255714800175 tuone namna ya kuonana tujadiliane namna rafiki ya kumaliza tatizo lako.
Ikiwa unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo niachie ujumbe WhatsApp +255714800175
SHARE POST HII NA RAFIKI ZAKO WENGINE