Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau, pilipili au tangawizi?

Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau, pilipili au tangawizi

Last Updated on 18/07/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau, pilipili au tangawizi?

Leo tena nijaribu kujibu swali hili kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo.

Ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa mara nyingi sana na wagonjwa wa vidonda vya tumbo.

Ukiwa unaumwa vidonda vya tumbo nguvu zako nyingi unazielekeza kwenye kutaka kufahamu ikiwa chakula hiki au kile kinaweza kuongeza maumivu ya vidonda au ikiwa kinaweza kukusaidia kupunguza maumivu na kusaidia kurahisisha kupona.

Hata hivyo usiwe bize sana kuhusu vyakula tu.

Kuna mengi zaidi kwenye vidonda vya tumbo zaidi ya vyakula na vinywaji.

Vidonda vya tumbo vinaweza kukujia kwa njia mbili.

Unaweza kupata vidonda vya tumbo kama matokeo ya kuwa na bakteria wa vidonda vya tumbo tumboni (H.Pyrol) lakini pia unaweza kupata vidonda vya tumbo kama matokeo ya kuzidi kwa asidi (tindikali) tumboni kwa kipindi kirefu.

Asidi inapozidi mwilini kwa kipindi kirefu huleta saratani mbalimbali.

Hii ndiyo sababu mara nyingi nasema hakuna sababu ya kuendelea kubembelezana na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu, hakuna sababu ya kuendelea kuvifanya vidonda vya tumbo kuwa ni sehemu ya maisha yako mwaka hadi mwaka.

Wakati ukiwa bize na upelelezi juu ya vyakula ni mhimu pia kwamba unapata dawa ya kukuponyesha kabisa na uendelee na maisha yako.

Bakteria wa vidonda vya tumbo unaweza kumpata kupitia maji unayokunywa au kupitia vyakula unavyokula.

Ukipata muda soma na hii > Mambo 6 niliyojifunza kuhusu vidonda vya tumbo.

Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau, pilipili au tangawizi?

1. Limau

Watu wengi hudhani kwa sababu limau lina ladha ya uchachu na ukali ukali basi halifai kuliwa na mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Na wengine ili kukupima kama una elimu au ufahamu kuhusu vidonda vya tumbo huwa wanapenda kuuliza swali ikiwa wanaweza kutumia limau ili waamue ikiwa wanunue dawa kwako au la.

Napenda kukujulisha kuwa ni kweli limau lina uchachu na lina asidi kama ambavyo ulifundishwa na watu wengine siku za huko nyuma.

Lakini kile unachopaswa kufahamu ni kuwa limau lina vitamini C nyingi sana, vitamini C ambayo ni nzuri kuliko ile ya kwenye chungwa na mgonjwa wa vidonda vya tumbo anahitaji sana vyakula vyenye vitamini C kwa wingi ili kumrahisishia kupona.

Lakini pia kile ulikuwa hujuwi ni kuwa limau linapokuwa mkononi mwako nje ya mwili wako ni kweli huwa na asidi na uchachu lakini unapokunywa maji maji ya limau na yanapofika tu tumboni hugeuzwa na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kutoka kuwa asidi na kuwa alkali (alkaline) hali ambayo tumbo la mgonjwa wa vidonda vya tumbo linaihitaji.

Kwahiyo limau ni baya kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo likiwa nje ya mwili, likiwa tumboni ni zuri sana, kwanza lina vitamini C ambayo ni mhimu sana ili kuimarisha kinga ya mwili na kutibu vidonda na majeraha pia linageuzwa na kuwa alkali mara tu lifikapo tumboni hali ambayo ni mhimu sana kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.

Tambua kwamba elimu haina mwisho na ingawa zamani mlikuwa mnaambiwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo anywe maziwa fresh lakini miaka ya karibuni imekuja kugundulika maziwa fresh si salama kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo.

Fungua akili yako na uwe mtu wa kujifunza kila mara.

Kwahiyo ukiniuliza mimi kama mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau jibu langu ni ndiyo anaweza kutumia.

Sasa ikiwa kwa upande wako ukitumia limau unapata maumivu zaidi basi nakushauri uanze kutumia kwa kiasi kidogo kidogo kwanza labda nusu kijiko kidogo cha chai kwa siku na ni vizuri uweke kwenye kitu kingine labda kwenye uji au kwenye juisi ya parachichi au kwenye supu ya mboga mboga.

Na ikiwa hampatani kabisa kwa vyovyote hata ukiweka kwenye vitu vingine basi nakushauri usitumie limau mpaka hapo utakapokuwa umepona kabisa vidonda vya tumbo lakini fahamu ni kitu unaweza kutumia na wapo wengine wanatumia.

2. Pilipili

Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau, pilipili au tangawizi

Pilipili nafahamu ndiyo kitu pekee kila mgonjwa wa vidonda vya tumbo aliyopo Tanzania anafahamu kwamba hatakiwi kabisa kutumia.

Hata mimi kwenye makala yangu ya vyakula ambavyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hatakiwi kutumia nimeiandika.

Nafahamu itakuwa ni vigumu kukushawishi kwamba unaweza kutumia pia pilipili wakati unaumwa vidonda vya tumbo!

Lakini huko nchini India pilipili ni kiungo mhimu kwenye vyakula vyao vyote.

Ukiwa India ni vigumu sana umalize siku asubuhi mpaka jioni hujatumia pilipili.

Wahindi ni walaji wakubwa wa pilipili duniani na cha kushangaza hawasumbuliwi na vidonda vya tumbo kama ilivyo hapa kwetu.

Na India ni taifa la pili lenye watu wengi zaidi duniani baada ya China.

Huko India tangu ukiwa mtoto wa miaka miwili utaanza kula pilipili mpaka uzee wako.

Wanasema kwa kawaida wahindi wakipandishiwa bei ya mafuta ya gari (diesel au petrol) hutawasikia wakipiga kelele yoyote lakini wakipandishiwa bei kidogo tu ya pilipili basi wanaweza kuandamana nchi nzima!

Hiyo ni kuonyesha ni jinsi gani wanavyoithamini pilipili na ni jinsi gani wanafahamu umhimu wake mwilini.

Kimsingi kabisa pilipili ni moja ya dawa za vidonda vya tumbo hasa vile vinavyoletwa na bakteria.

Hakuna bakteria anaweza kubaki salama mbele ya pilipili na ndiyo sababu wahindi wengi hawaumwi vidonda vya tumbo kwa sababu tayari wanavidhibiti kupitia pilipili wanayoweka kwenye chakula.

Kwahiyo mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza pia kutumia pilipili lakini unashauriwa kuianza pole pole na uitumie kidogo sana kwa siku za mwanzoni.

Kwa sababu pilipili ni dawa nzuri dhidi ya bakteria (antibacteria) na hakuna bakteria hata huyo wa vidonda vya tumbo anaweza kubaki salama mbele ya pilipili.

Lakini pia kama ilivyo kwa limau, hata pilipili pia ikiwa ukiitumia inaamsha maumivu zaidi nakushauri usiitumie mpaka hapo utakapokuwa umepona kabisa vidonda vyako.

Lakini pilipili bado siyo haramu kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, ni dawa, pia ni kinga ya vidonda vya tumbo hasa vile vinavyotokana na bakteria.

Labda hapa nitoe tu angalizo kuwa pilipili nzuri ni ile fresh au ya nyumbani, epuka pilipili za dukani zilizosindikwa viwandani kwani huongezwa vitu vingine visivyofaa ili kuifadhi isiharibike kwa muda mrefu.

3. Tangawizi

Tangawizi na vidonda vya tumbo

Tangawizi ni dawa pia ya vidonda vya tumbo.

Tangawizi ni mdhibiti mzuri dhidi ya bakteria wengi hasa wale wa tumboni na pia tangawizi inao uwezo wa kudhibiti asidi mwilini.

Kwahiyo tangawizi inatibu vidonda vya aina zote 2 yaani vile vinavyoletwa na bakteria na vile vinavyoletwa na asidi.

Tangawizi ni dawa nzuri karibu kwa kila tatizo la tumboni.

Ni dawa kwa miaka mingi na imekuwa ikitumika kwa karne na karne kutibu maradhi mbalimbali hasa yale ya tumboni.

Jambo la mhimu kuhusu tangawizi hasa kwa wewe mgonjwa wa vidonda vy atumbo ni kuitumia kwa kiasi na ikiwezekana upate tangawizi mbichi na siyo ile ya unga.

Tangawizi mbichi ni nzuri zaidi kuliko ya unga na kwa wewe mgonjwa wa vidonda vya tumbo nakushauri uwe unaitumia sambamba na vitu vingine hasa hasa itumie sambamba na juisi ya parachichi iliyoungwa asali.

Kwahiyo ni juisi ya parachichi + asali + tangawizi kidogo.

Unaweza kutumia jusi yoyote ya matunda iliyoandaliwa nyumbani lakini usisahau kuongeza asali na tangawizi kidogo mbichi.

Tangawizi hiyo unaweza kuisaga pamoja kwenye blenda sambamba na matunda ya hiyo juisi yako.

Kama kawaida anza nayo kidogo kwa mbali hasa ikiwa wewe unasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Tambua tangawizi siyo haramu kwako mhimu tu uichukue kidogo kidogo na pole pole huku ukiichanganya na vitu vingine kama juisi, uji, na mboga za majani.

Na ikiwa kwa upande wako ukitumia tangawizi mambo yanaamka zaidi tafadhali iache hadi hapo utakapokuwa umepona kabisa.

Faida nyingine za tangawizi mwilini;

1. Huondoa sumu mwilini haraka sana

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi

3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi

4. Huondoa uvimbe mwilini

5. Huondoa msongamano mapafuni

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake

7. Huondoa maumivu ya koo

8. Huua virusi wa homa

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini

10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi

19. Huongeza msukumo wa damu

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo

21. Huzuia damu kuganda

22. Hushusha kolesto

23. Husafisha damu

24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa

25. Hutibu shinikizo la juu la damu

26. Husafisha utumbo mpana

27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma

28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI

29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu

31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa

33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula

34. Husaidia kuzuia kuharisha

35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu

36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto

37. Hutibu homa ya kichwa

38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi

39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito

40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

41. Huimarisha afya ya figo

42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi

43. Ina madini ya potassium ya kutosha

44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha

46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium

47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene

48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita.

Ikiwa una kitu kingine ambacho huelewi ikiwa unapaswa kula au la naomba uulize hapo chini kwenye sanduku la comment na mimi nitakujibu tena hapa hapa BURE.

Ikiwa unahitaji dawa ya asili inayotibu kabisa vidonda vya tumbo bonyeza hapa.

WhatsApp natumia +255714800175

Share post hii na wengine uwapendao.

Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau, pilipili au tangawizi Share on X
Imesomwa na watu 518
Je mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kutumia limau, pilipili au tangawizi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *