Chakula cha mgonjwa wa bawasiri

Last Updated on 27/06/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

Chakula cha mgonjwa wa bawasiri

Mgonjwa wa bawasiri unashauriwa kuwa makini sana na chakula unachokula kila siku.

Chakula na vinywaji unavyotumia kila siku vina mchango mkubwa katika kukusaidia kupona ugonjwa huu unaosumbuwa maelfu ya watu miaka ya sasa kote duniani.

Chakula cha mgonjwa wa bawasiri kinafaa kifanane na kile cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Mara nyingi nimeandika hapa kwamba kuna uhusiano wa karibu sana kati ya bawasiri na vidonda vya tumbo na upungufu wa nguvu za kiume.

Kwahiyo unapoumwa bawasiri tambua kwamba vidonda vya tumbo vipo karibu sana kwako na huenda tayari unavyo ila tu bado hufahamu.

Kwa kawaida mgonjwa wa bawasiri unashauriwa kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi (high fiber rich foods) lakini vile vile mhimu kuzingatia kuwa kama bawasiri yako inatokana na kupata choo kigumu kwa muda mrefu au mara kwa mara unatokewa na hali ya kupata choo kigumu basi utatakiwa kuongeza vyakula vya nyuzinyuzi pole pole.

Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi kwa wingi kwa ghafla kunaweza kukuletea tatizo la gesi kujaa tumboni au mvurugiko tu usiofaa wa tumbo.

Tafiti mbalimbali zinasema vyakula vyenye nyuzinyuzi vinaweza kupunguza maumivu yatokanayo na bawasiri kwa zaidi ya asilimia 50 na husaidia mgonjwa kupona haraka na kuzuia tatizo la bawasiri lisijirudie tena siku za mbeleni.

Vyakula vyenye nyuzinyuzi hukusaidia kupata choo kila siku na unapata choo kilaini bila maumivu yoyote.

Isipite siku yoyote hujapata choo japo mara moja na ukiweza kupata mara 2 au 3 basi ni vizuri zaidi.

Unashauriwa kukaa mbali na vilevi vyote, kuacha kula vyakula vya dukani na vile vya kwenye makopo na kwenye migahawa (fast foods and take aways).

Kama unapenda kujifunza vyakula vingine ambavyo mgonjwa wa bawasiri hatakiwi kula bonyeza hapa.

Penda zaidi kula chakula cha asili na maji mengi kila siku.

Usinywe maji zaidi ya lita 3 na nusu kwa siku labda kama unafanya kazi ngumu inayokutoa jasho jingi.

Chakula cha mgonjwa wa bawasiri.

Kama unaumwa bawasiri nakushauri ule kwa wingi vyakula vifuatavyo kila siku ;

1. Mboga za majani nyingi kila siku. Mboga za majani nyingi. Mboga za majani nyingi.

2. Matunda hasa parachichi, ndizi za kuiva, papai, tufaa na mapeazi.

3. Karoti, maboga, Vitunguu swaumu, vitunguu maji, pilipili hoho, bamia, viazi vitamu na viazi vya chips vya kuokwa kwenye oven na bila kumenya ngozi yake.

4. Maharage, kunde, dengu, na njegele.

5. Mbegu mbegu kama vile mbegu za maboga, almond, mbegu za alizeti na mbegu mbegu zingine.

6. Ugali wa dona, mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread), samaki, kuku, mayai (jaribu vegetable omelets)

7. Asali, mtindi, tui la nazi (kikombe kimoja kila siku), na uji wa Unga wa ndizi.

8. Supu za mboga mboga nk

Kama wewe ni mbunifu unaweza kupata vyakula vingi (receips) vya asubuhi, mchana na jioni kulingana na nilivyovitaja hapa.

Vile vile siyo lazima chakula cha mchana au cha usiku kiwe na ugali au wali kama wengi mlivyozoea.

Unaweza kula samaki na mboga za majani nyingi na ukashiba bila ugali wala wali, au ukala nyama na mboga za majani nyingi bila ugali wala wali na ukashiba.

Unaweza pia kuamua mlo mmoja ama wa asubuhi au wa usiku uwe ni matunda tu peke yake bila ugali wala wali.

Penda kupika vyakula vyako vyote kwa kutumia tui la nazi au mafuta ya zeituni.

Ukiwa na swali zaidi niulize hapo chini kwenye boksi la comment na mimi nitakujibu tena hapa hapa BURE.

Kama unapenda kujifunza mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa bawasiri bonyeza hapa.

Chakula cha mgonjwa wa bawasiri Share on X
Imesomwa na watu 2,613
Chakula cha mgonjwa wa bawasiri

One thought on “Chakula cha mgonjwa wa bawasiri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *