Kwanini mgonjwa wa bawasiri unashauriwa kuacha kunywa pombe

Last Updated on 15/01/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Kwanini mgonjwa wa bawasiri unashauriwa kuacha kunywa pombe

Moja ya magonjwa yanayoendelea kusumbua watu ni ugonjwa wa bawasiri.

Baada ya u.t.i, vidonda vya tumbo, ugonjwa wa tatu unaotesa watu wengi duniani kwa sasa ni ugonjwa wa bawasiri.

Shida iliyopo ni kuwa ugonjwa huu upo sehemu mbaya na wengi huona aibu kujieleza kuwa wanaumwa bawasiri na hivyo huchelewa sana kupata matibabu.

Kadri unavyoendelea kuumwa muda mrefu bawasiri na ukaendelea kuchelewa kutafuta tiba yake ndivyo ugonjwa huu unavyozidi kuwa sugu na ndivyo inavyokuwa shida kupona.

Bawasiri ni ugonjwa kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, ni ugonjwa wenye uhusiano wa karibu na vidonda vya tumbo na mara nyingi mtu mwenye bawasiri ana vidonda vya tumbo pia au mwenye vidonda vya tumbo ana bawasiri pia.

Bawasiri na Vidonda vya tumbo ni mtu na kaka yake.

Bawasiri ni hali ya mtu kukosa Choo kwa muda mrefu au kupata Choo kigumu kila mara, kupata Choo chenye damu, kupata Choo kwa maumivu na mwishoni kabisa kinyama au vinyama na vivimbe kadhaa hujitokeza sehemu ya haja kubwa.

Bawasiri kama bawasiri ni tatizo lililopo ndani tumboni kwa mtu, ni tatizo linaloanzia ndani tumboni.

Ni ishara kuna kitu si sawa kwenye afya yako ya tumbo na mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula kwa ujumla.

Kwa bahati mbaya dawa peke yake siyo suluhisho la kudumu na la uhakika ili kutibu bawasiri.

Ndiyo maana tayari umetumia dawa nyingi za kunywa na za kupaka lakini bado huponi au unapata nafuu ya muda mfupi lakini tatizo linarudi tena.

Ili kupona bawasiri ni lazima mgonjwa awe makini juu ya;

1. Chakula,

2. Vinywaji na

3. Aina ya maisha anayoishi kila siku.

Bila kuzingatia mambo matatu hapo juu kupona na kuiondoa kabisa bawasiri itakuwa ni kazi ngumu sana.

Moja ya vinywaji mgonjwa wa bawasiri unashauriwa kuacha kunywa ni pamoja na pombe.

Ndiyo, kama unaumwa na kusumbuliwa na bawasiri kwa kipindi kirefu unashauriwa kunywa pombe kistaarabu na ukiweza acha kwanza kunywa pombe kwa miezi mitatu mpaka sita ili kuuongezea mwili wako uwezo wa kupigana na ugonjwa na hatimaye upate uponyaji.

Sababu kuu ya mgonjwa wa bawasiri kushauriwa kuacha kunywa pombe ni kuwa pombe ina matokeo mengine mabaya ambayo ni kukausha maji mwilini.

Pombe hufanya kazi kama kikojoshi yaani ‘diuretic’ na hivyo hukulazimisha kwenda kupata haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida.

Ukinywa pombe nusu lita kuna uwezekano wa wewe kwenda kukojoa mkojo wa ujazo wa lita 1 ndani ya muda mfupi tangu unywe pombe.

Jambo hilo hutokea pia unapokunywa kwa wingi vinywaji vyenye kaffeina kama vile kahawa, chai ya rangi, soda za energy, soda nyeusi zote na cocoa.

Hakuna kitu mgonjwa wa bawasiri anahitaji mwilini mwake kama maji.

Maji mwilini ni mhimu sana kwa mgonjwa wa bawasiri ili kumsaidia asipate choo kigumu, ili kumsaidia asikose choo kila siku na kumrahisishia uponyaji kwa ujumla.

Pombe inakausha maji mwilini na kufanya hali yako ya bawasiri kuwa mbaya zaidi na kuzuia uponyaji kutokea.

Kumbuka mwamuzi wa mwisho kuhusu afya yako ni wewe mwenyewe, inakuhusu wewe. Sisi wengine ni washauri tu.

Kila mara popote ulipo kama unaumwa bawasiri uwe na chupa ya maji ya kunywa pembeni yako na unywe tu maji mara kwa mara bila kusubiri kiu.

Wakati huo huo kunywa pombe kupita kiasi kunaweza kukuletea shinikizo la juu la damu ambalo nalo linaathiri vipenyo vya mishipa ya damu ambayo inatakiwa kusambaza maji sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo mishipa kwenda kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na utoaji taka mwilini.

Pombe pia inaweza kuleta kuongezeka kwa mapigo ya moyo ambayo na yenyewe yanakausha maji zaidi mwilini na pengine kukusababishia tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Kuna uhusiano pia wa unywaji wa pombe na matatizo ya ini. Na ini linahusika na uondoaji wa taka na sumu mbalimbali mwilini na mgonjwa wa bawasiri anatakiwa kuwa na mfumo wa uondoaji taka mwilini unaofanya kazi vizuri na ufanisi wa hali ya juu.

Kama umekuwa ukisumbuliwa na bawasiri kwa muda mrefu na unakunywa pombe na vilevi vingine, unashauriwa kupunguza sana kunywa pombe na ukiweza acha kwanza kunywa pombe mpaka hapo utakapokuwa umepona bawasiri.

Ikiwa unahitaji dawa nzuri ya asili kwa ajili ya kutibu bawasiri niachie tu ujumbe WhatsApp 0714800175

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 313
Kwanini mgonjwa wa bawasiri unashauriwa kuacha kunywa pombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *