Hadithi 8 za uongo kuhusu bawasiri

Last Updated on 17/11/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Hadithi namba 1: Ukiugua bawasiri hata ukipona utarudia kuugua tena na tena.

Ukweli ni upi: Madai haya hayana ukweli wowote hasa kwa yule ambaye amepata ugonjwa huu kwa sababu za muda mfupi tu kama vile ujauzito.  

Kwa kawaida ukitibiwa ugonjwa huu na ukapona kitakachosababisha upate tena ugonjwa huu ni kutokuzingatia masharti unayopewa juu ya vyakula na namna ya kuishi kwa ujumla ili kujikinga na tatizo lisijirudie tena.

Hata baada ya kupona bado unatakiwa uendelee kula vizuri na kuishi vizuri wakati wote ili kwamba usipate tena ugonjwa huu.

Ni ugonjwa wa tabia na hivyo kadri unavyojiepusha na tabia zinazopelekea ugonjwa huu ndivyo unavyojiweka mbali na kuugua tena.

Hadithi: Bawasiri inaweza kuleta saratani ya utumbo mpana

Ukweli ni upi: Bawasiri kama bawasiri haiwezi kukuletea saratani ya utumbo mpana.

Hata hivyo dalili za bawasiri zinafanana sana na zile za ugonjwa wa saratani ya utumbo mpana (colon cancer).

Kwahiyo ni mhimu sana kwamba unahangaika kwa vyovyote utakavyoweza kupata matibabu kwa ajili ya bawasiri mapema wakati inapojitokeza na siyo kusubiri mpaka hali iwe mbaya kiasi cha kufananishwa na saratani.

Hadithi: Ninakula vyakula vya nyuzinyuzi hivyo siwezi kuugua bawasiri

Ukweli ni huu: Wakati kula vizuri hasa kupendelea kula vyakula vyenye nyuzinyuzi ni hatua nzuri ya kujikinga usipatwe na bawasiri bado hilo pekee halizuii wewe kuugua ugonjwa huu.

Kuna sababu zingine kuu zinazoleta ugonjwa huu ikiwemo tabia ya kukaa tu chini au kwenye kiti masaa mengi, kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi ya kutosha kila siku.

Hadithi: Kuendesha baiskeli muda mrefu kunaweza kusababisha bawasiri.

Ukweli: Miaka mingi mababu zetu wamekuwa wakitegemea baiskeli kama usafiri wao mkuu na hawakuugua bawasiri kama tunavyoteseka sisi miaka ya sasa.

Kuendesha baiskeli kunaweza kusikuletee bawasiri moja kwa moja ila kunaweza kuwa ni sababu mojawapo ya kutokea kwa dalili au hatua za mwanzo za bawasiri.

Kama unaendesha baiskeli lakini unakula vizuri na baadaye unakuwa unatumia muda mwingi kusimama au kutembeatembea na siyo kukaa tu kwenye kiti kuna uwezekano mdogo wa wewe kupatwa na bawasiri.

Kinachosaidia ni kwamba baiskeli tofauti na pikipiki au gari baiskeli ni sehemu ya mazoezi pia kwa mwili hivyo kuna faida za kiafya unaweza kuzipata ambazo zitakusaidia usipate bawasiri kirahisi kama vile ungekuwa boda boda au dereva wa gari.

Hadithi: Ni watu wazima tu ndiyo hupata bawasiri

Ukweli: Ingawa ni kweli ugonjwa huu kwa sehemu kubwa umekuwa ukionekana mara nyingi ukiwatokea watu wazima bado haimaanishi kwamba ni watu wazima tu ndiyo wanaougua ugonjwa huu.

Ukweli ni kuwa mtu wa umri wowote ambaye muda mwingi anatumia kukaa chini au kwenye kiti, hali vyakula vingi vya nyuzinyuzi (fiber) na anakula zaidi vyakula feki anaweza kupata ugonjwa huu bila kujali umri wake.

Kwahiyo watoto na hata watu wazima wazee sana pia wote wanaweza kupatwa na ugonjwa huu.

Ugonjwa huu unaonekana kuwatesa zaidi wanawake kuliko wanaume sababu ya tabia yao ya kupenda kukaa muda mrefu kwenye kiti na wengine kwa sababu zinazotokana na ujauzito.

Hadithi: Mara zote bawasiri huambatana na kutoka damu

Ukweli unasemaje: Madai haya tena hayana ukweli. Dalili za bawasiri zinaweza kutokea bila kuhusisha kutoka damu wakati wa kujisaidia.

Kuna bawasiri za aina mbili hasa ambazo ni bawasiri ya ndani na bawasiri ya nje na zote mbili siyo lazima zipelekee kuvuja damu.

Kwenye bawasiri ya nje uvimbe unaweza kusikika na kuonekana sehemu ya nje ya tundu la haja kubwa na inaweza kuleta maumivu wakati unajisaidia lakini siyo lazima iambatane na damu.

Ikikutokea kwamba bawasiri yako inaambatana na kutokwa damu utahitaji matibabu ya haraka zaidi kwani unaweza kupatwa na madhara mengine mabaya zaidi kiafya yatokanayo na damu kupungua kwa kupotea hivyo pole pole kila siku.

Hadithi: Bawasiri haiponi mpaka ufanye upasuwaji.

Ukweli ni: Upasuwaji (operation) siyo njia pekee ya kutibu tatizo hili. Upasuaji ni njia ya haraka (quick fix) ya kuondoa uvimbe wa bawasiri ya nje. Hapa unakuwa umeondoa uvimbe uliotokana na bawasiri na siyo bawasiri yenyewe.

Bawasiri ni ugonjwa unaoanzia ndani ya mwili tumboni kwenye mmeng’enyo wa chakula.

Uonapo uvimbe kwenye sehemu ya tundu la haja kubwa hiyo siyo bawasiri, huo ni uvimbe kama matokeo ya bawasiri.

Pamoja na upasuaji ili kuondoa uvimbe bado utahitaji kula vizuri na kutumia baadhi ya dawa za kunywa ili kwamba chanzo cha ugonjwa wenyewe kilichojiunda tumboni kiweze kupotea ili kwamba usiendelee tena kuugua ugonjwa huu.

Utakuwa shuhuda hapa kwamba umeshawahi kufanya upasuaji na bado wiki kadhaa mbeleni uliona uvimbe ukijirudia tena na ukabaki unashangaa.

Hadithi: Bawasiri ni ugonjwa usiotibika

Ukweli upoje: Ni ugonjwa wa kawaida na unatibika na kupotea.

Inawezekana umeshatumia dawa za kila namna na huoni dalili zozote za kupona.

Bado kuna watu wanapona bawasiri hasa wale wanaozingatia maelezo wanayopewa na matabibu juu ya vyakula na namna ya kuishi kwa ujumla.

Ni wale tu wanaoweka matumaini yote kwenye dawa bila kujibidiisha kubadili vyakula na mifumo yao ya maisha inayopelekea ugonjwa wa bawasiri ndiyo hawaponi.

Hata kwa upande wa vidonda vya tumbo kuna imani za namna hii kwamba ni ugonjwa usiotibika. Siyo kweli, wapo wanaopona na mimi ninazo shuhuda za watu wanaopona bawasiri hata vidonda vya tumbo. Usikae tu na kuishi na ugonjwa wowote, chukua hatua.

Hitimisho

Bawasiri ni ugonjwa wa kawaida na unatibika.

Tofauti na unavyoweza kufikiri na pengine hata kuona aibu, ni kuwa ugonjwa huu wanaugua watu wengi sana na hauchagui maskini wala tajiri.

Ni ugonjwa wa pili unaotesa watu wengi baada ya U.T.I na una uhusiano wa karibu na vidonda vya tumbo.

Upatapo ugonjwa huu usione aibu, chukua hatua mapema ili kuweza kupona kirahisi kuliko ukisubiri hali iwe mbaya zaidi kiasi cha matibabu kukugharimu zaidi na kuchukuwa muda mrefu kuliko kawaida.

Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu bawasiri niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Kama unapenda kujifunza mengi zaidi kuhusu ugonjwa wa bawasiri bonyeza HAPA.

SHARE post hii kwa ajili ya wengine.

Imesomwa na watu 602
Hadithi 8 za uongo kuhusu bawasiri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *